Zaidi ya watu 717 waliokuwa wakishiriki sherehe za hija wamefariki baada
kutokea mkanyagano karibu na mji wa mtakatifu wa Kiislamu wa Mecca.
Idara ya ulinzi wa
raia nchini Saudi Arabia imesema kuwa watu wengine 863 wamejeruhiwa katika kisa
hicho kilichotokea eneo la Mina, takriban kilomita tano kutoka mji wa Mecca.
Maafa hayo yalitokea
mahujaji takriban milioni mbili walipokuwa wakishiriki moja ya kaida muhimu za
mwisho katika ibada za hija.
Huu ni mkasa mbaya
zaidi kutokea wakati wa hija katika kipindi cha miaka 25.
Mahujaji husafiri hadi
Mina wakati wa kuhiji kurusha mawe saba kwenye nguzo saba zijulikanazo kama
Jamarat, ambazo huwakilisha shetani.
Nguzo hizo zimo katika
eneo ambalo inaaminika Nabii Ibrahim alijaribiwa na shetani.
Watu walikuwa
wakielekea eneo la kurushia mawe, na wengine wakitokea huko na pale ghafla watu
walipoanza kuanguka.
Kulikuwa na raia wa
Nigeria, Niger, Chad na Senegal miongoni mwa mataifa mengine.
Idara ya ulinzi wa
raia Saudi Arabia imesema mkanyagano huo ulitokea pale kulipotokea ongezeko la ghafla
la watu waliokuwa wakielekea kwenye
nguzo za kurushiwa mawe.
Waziri wa afya wa
Saudi Arabia Khaled al-Falih amesema mkanyagano huo ulitokea kwa sababu
mahujaji walikosa kufuata maagizo.
"Wengi wa
wahamiaji huenda bila kufuata ratiba iliyowekwa," alisema.
Hata hivyo Idara ya
ulinzi wa raia Saudi Arabia imesema maafisa 4,000 wametumwa eneo hilo kusaidia
pamoja na wahudumu 200 wa huduma za dharura.
Maandalizi ya ibada
hizo za hija yalikuwa yamekumbwa na mkasa baada ya kreni kuanguka katika
msikiti mkuu wa Mecca mwezi huu na kuua watu 109,hii si mara ya kwanza kwa
mikasa kutokea wakati wa hija.
Mikasa mingine
iliyotokea wakati wa kuhiji:
2006: Mahujaji 364
walifariki wakati wa kurushia mawe mnara unaoashiria shetani
1997: Mahujaji 343
walifariki na 1,500 kujeruhiwa kwenye mkasa wa moto
1994: 270 waliuawa
katika mkanyagano
1990: Mahujaji 1,426
waliuawa katika mkanyagano njia za kupitia chini za kuelekea maeneo matakatifu
1987: Watu 400
walifariki maafisa wa serikali walipokabiliana na waandamanaji waliounga mkono
Iran.
Chanzo BBC.
No comments:
Post a Comment