![]() |
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam limejipanga kikamilifu
kuhakikisha kuwa pambano la mpira wa miguu kati timu za SIMBA na YANGA ambalo
linavuta hisia za mashabiki wengi wa hapa Tanzania linafanyika katika hali ya
amani na usalama.
Mchezo ambao unatarajia kufanyika katika dimba la taifa jijini dar es
salaam tarehe sept 27 mwaka huu,Hivyo
mashabiki wanashauriwa wasiwe na shaka yoyote ya kiusalama lakini wanatakiwa kutoa
ushirikiano kwa kutoa taarifa za jambo lolote watakaloliona kuwa linaweza
kuwa chanzo cha uvunjifu wa amani kwa kipindi chote watakapokuwa nje au ndani
ya uwanja wa taifa.
Katika mchezo huo Kutakuwa na askari wa kutosha ambao watazunguka maeneo yote muhimu ya uwanja huo kwa lengo la kuimarisha ulinzi muda wote ambao uku askari wengine watakuwa katika milango mikuu ya kuingilia na ndani ya uwanja .
Sanjali na haya kutakuwa na ulinzi wa kutumia camera (CCTV Camera) zitakazofungwa kuzunguka uwanja huo ili kusaidia kuimarisha ulinzi katika mechi hiyo muhimu, hivyo matukio yote yatakayokuwa yanatokea yatarekodiwa.

No comments:
Post a Comment