MCHEZAJI WA WESTHAM UTD MARK NOBLE , NDIYE ANAONGOZA KUCHEZEWA FAULO MPAKA SASA. - WINGU LA HABARI- ONLINE

Breaking

TANGAZO

TANGAZO
Sugar free

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Friday, September 25, 2015

MCHEZAJI WA WESTHAM UTD MARK NOBLE , NDIYE ANAONGOZA KUCHEZEWA FAULO MPAKA SASA.

Mchezaji wa Westham Utd Mark Noble akiwa  katika haraka
za kushangilia bao.














Mchezo wa mpira wa miguu ni mchezo unaopendwa na  watu wengi ukilinganisha na michezo mingine , lakini mchezo huo licha kupendwa na watu wengi kuna changamoto kadha kwa namna moja ama  nyingine ambazo wachezaji wanakutana nazo . 

Miongoni mwa changamoto hizo ni pamoja na kuchezewa madhambi na  mchezaji mwezako jambo ambalo linaonekana  ni  la kawaida  katika mchezo lakini  wakati mwengine  mchezaji umgalimu katika maswala mbalimbali  ikiwemo katika utendaji na nafasi yake katika kuhakikisha timu inapata matokeo.

Msomaji wa  Wingu la habari leo nakuletea orodha ya wachezaji  kadha ambao wamechezewa madhambi mara nyingi kuliko wachezaji wengine unaowajua katika  ramani  ya  soko hapa duniania, katika  msimu mpya wa ligi ya Uingereza ,  na miongoni mwa wachezaji hao ni pamoja  na  mchezaji wa West Ham UTD Mark Noble, huyu ndio mchezaji anayeongoza kwa kufanyiwa madhambi katika ligi kuu Uingereza mpaka sasa.

Kwani amefanyiwa madhambi mara 19 katika michezo 6 aliyocheza tangu msimu mpya uanze, ukiwa ni wastani wa rafu 3.2 kwa mechi alizocheza.

Mchezaji wa pili Andre Ayew wa Swansea ambaye amefanyiwa madhambi mara 18, ukiwa ni wastani wa faulo 3 kwa kila mchezo.Wa tatu ni Alexis Sanchez amefanyiwa mara 17 mpaka sasa kwa uwiano wa 2.8 kwa mechi.

Eden Hazard amefanyiwa mara 16 akiwa na  uwiano wa  2.7 kwa mechi, wakati Ross Barkley na Sadio Mane wakiwa wamefanyiwa faulo mara 15, ukiwa ni uwiano wa 2.5 .

Na mchezaji  Idrissa Gueye wa Aston Villa amefanyiwa madhambi mara 12, ukiwa ni wastani wa faulo 3 kwa kila mechi.

Historia inaonyesha kuwa msimu wa mwaka jana, Eden Hazard ndio alikuwa  mchezaji aliye fanyiwa faulo nyingi zaidi, mara 113, ukiwa ni uwiano wa 3 kwa mechi.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here