PAPA FRANCIS AWASILI NEW YORK, TAYALI KULIHUUTUBIA BARAZA LA UMOJA MATAIFA - WINGU LA HABARI- ONLINE

Breaking

TANGAZO

TANGAZO
Sugar free

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Friday, September 25, 2015

PAPA FRANCIS AWASILI NEW YORK, TAYALI KULIHUUTUBIA BARAZA LA UMOJA MATAIFA

Papa Francis akiwasili New York katika uwanja
wa ndege .














Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis amewasili mjini New York na anatarajiwa kulihutubia baraza kuu la Umoja wa Mataifa baadaye leo.

Papa aliwasili Manhattan baada ya safari fupi kutoka uwanja wa ndege wa John F. Kennedy kwa njia ya helikopta.

Kiongozi huyo alihudhuria ibada ya maombi kwa watu takriban 2,500 katika kanisa la Mtakatifu Patrick na katika ratiba yake ya leo yenye shughuli nyingi Papa Francis atawahutubia viongozi katika Umoja wa Mataifa na kushiriki ibada ya dini mbalimbali katika jumba la makumbusho la mashambulizi ya Septemba 11, 2001 eneo la Ground Zero jijini New York.

Akiwa new York ataongoza misa katika uwanja wa Madison Square Garden na kutembea katika bustani ya katikati ya mji huo.

Kiongozi huyo wa kanisa Katoliki duniani aliwasili New York akitokea Washington ambako alilihutubia bunge la Marekani na kuwahimiza wabunge wafanye juhudi zaidi kupambana na ugaidi wa kimataifa.

Chanzo DW.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here