Kushindwa huko kumefikia kikomo cha rekodi yao ya kushinda mechi
zao zote msimu huu.
Katika mchezo huo Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool Iago Aspas
alifunga mabao mawili baada ya Nolito kuanza kufunga mabao dhidi ya klabu hiyo
yake ya zamani.
Neymar aliipatia Barcelona bao moja la kufutia machozi zikiwa zimesalia
dakika 10 kabla ya mchezo huo kuisha.
Barcelona walikuwa wamepoteza mechi moja pekee kati ya 25
walizocheza majuzi katika La Liga.
Ushindi wa Celta uliwaweka kileleni mwa ligi kwa muda, lakini
Real Madrid waliwabandua baadaye baada ya kulaza Athletic Bilbao.
Kufatia matokeo hayo mkufunzi mkuu wa Barca Luis Enrique alisema
kuwa Kilichoamua mechi hii ni jinsi ya
Celta walivyocheza vyema na kupata ushindi.
Aidha
alisema kuwa katika mchezo walijalibu kushindana ulijaribu kushindana lakini
waliwazidi ujanja .
’’Timu
inapokuwa bora na kukushinda, huwa huna mengi ya kusema, hivyo heri nishindwe na timu inayocheza kama
Celta walivyocheza leo, bila kutumia hila, kushinda kwa kucheza vyema soka, nawapongeza
na natumai waendelee kucheza hivyo hivyo.”alisema
Kufungwa
kwa Barcelona magoli manne ni mara ya tatu katika mechi tisa walizocheza msimu
huu kwani Walilazwa 4-0 na Athletic Bilbao katika Super Cup ya Uhispania na pia
walicharaza Sevilla 5-4 katika Super Cup ya Uefa.

No comments:
Post a Comment