![]() |
| MWILI WA MAREHEMU MH BI CELINA KOMBANI UKIWA UMEBEBWA TAYALI KWA KUZIKWA |
Wananchi wa mkoa
wa Morogoro wamepokea kwa majonzi msiba wa aliyekuwa waziri wa nchi ofisi ya
rais menejimenti ya utumishi wa umma na mbunge wa jimbo la Ulanga Bi, Celina
Kombani mazishi yaliofanyika leo katika eneo la shamba lake lililopo Lukobe
manispaa ya Morogoro.
Wakizungumza nyumbani kwa marehemu wakazi wa
Morogoro wameeleza kusikitishwa na msiba huo ambapo wamesema marehemu alikuwa
kipenzi cha watu, mchapa kazi na kuwataka wakazi wa Morogoro hususani wa jimbo
la Ulanga kuwa wavumilivu kwa kupotelewa na kipenzi chao ambapo waziri huyo
alikuwa anagombea ubunge kwa awamu ya tatu kwa tiketi ya CCM katika jimbo la
Ulanga.
Wakizungumza kwa niaba ya
familia kaka wa marehemu Martin Ombeshi na mkwe wa marehemu Bw, Jeradi Mlenge
wamesema wameupokea msiba huo kwa masikitiko ambapo wameeleza mazishi hayo
yamefanyika leo mkoani Morogoro shambani
kwake Lukobe
![]() |
| Waziri wa nchi ofisi ya rais menejimenti ya utumishi wa umma na mbunge wa jimbo la Ulanga Bi, Celina Kombani kipindi cha uwahi wake. |
![]() |
Waziri mkuu Mzengo Pinda akitoa salama za mwisho
|



No comments:
Post a Comment