Akiongea na wanahabari kuhusu mechi ya leo kati ya kilabu yake
na Porto ya Ureno katika Ligi ya Kilabu Bingwa Ulaya, Mourinho alisema kuna
hamu kubwa ya kumsimamisha au kumpiga marufuku mchezaji huyo miongoni mwa
waamuzi.
Costa alipigwa marufuku mechi tatu na Shirikisho la Soka la
Uingereza baada ya kupatikana na hatia ya utovu wa nidhamu wakati wa mechi dhidi
ya Arsenal ligi kuu.
Lakini yuko huru kucheza dhidi ya Porto leo kwani marufuku hiyo
haigusi mechi za Ulaya.
Alipoulizwa iwapo angelipenda kuwa na wachezaji 11 walio kama
Costa uwanjani, Mourinho alisema: “Tungeshindwa kila mechi, kwa sababu hamu ya
kumpiga marufuku iko juu mno kiasi kwamba tungekosa wachezaji wa kuanza nao
mechi.”
“Nina furaha tu kwamba kwa sasa nina mmoja tu na mwache acheze
hadi waamue kumpiga marufuku tena.”
Costa amekosa mechi mbili Uingereza, na pia atakosa mechi ya
wikendi dhidi ya Southampton.
Kwenye kikao hicho na wanahabari, Mourinho pia alionya wachezaji
wake kwamba hakuna aliye salama iwapo kilabu hiyo itaendelea kuandikisha
matokeo mabaya.
Mourinho amekuwa akimuweka benchi John Terry mechi mbili
zilizopita za Ligi ya Premia, ihali Branislav Ivanovic na Cesc Fabregas pia
wamekosolewa kutokana na uchezaji wao.
"Watu wasioguswa, ni uendelevu pekee unaoweza kukupa hadhi
hiyo,” alisema Mourinho, ambaye vijana wake wamo nambari 14 ligini baada ya
mechi saba kucheza.
No comments:
Post a Comment