![]() |
| kipa mahili Gianluigi buffon akiwa katika majukumu yake ya kazi. |
Kipa nyota wa duniani Gianluigi Buffon ameweka
wazi mapenzi yake ya dhati juu ya kipa mwezake mwingine Iker Casillas.
Buffon amesema Casillas
ni kipa bora kwa ngazi ya klabu na taifa, lakini anashangazwa na mambo
yalivyobadilika kwake haraka na wengine kufikia kumvunjia heshima kwa kumzomea,
jambo ambalo anaamini si sahihi hata kidogo.
"Navutiwa sana na Casillas, ameshinda kila kitu katika
mpira. Anajua kila kitu katika mpira na amekuwa mtu bora na mpambanaji wa
dhati.
“Anastahili heshima kubwa, kwangu hata kama angepiga mpira
uingie langoni na kujifunza, bado hastahili kuzomewa, apigiwe makofi,” alisema
Buffon.
Baada ya kuona mambo yake hayaendi vizuri na Real Madrid,
Casillas aliamua kuondoka na kujiunga na FC Porto na leo atakuwa uwanjani timu
yake ikicheza na Chelsea.

No comments:
Post a Comment