IDADI YA WATU WANOTUMIA HUDUMA YA SIMU KUNUNUA NA KUUZA HISSA YAONGEZEKA. - WINGU LA HABARI- ONLINE

Breaking

TANGAZO

TANGAZO
Sugar free

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Tuesday, September 29, 2015

IDADI YA WATU WANOTUMIA HUDUMA YA SIMU KUNUNUA NA KUUZA HISSA YAONGEZEKA.

Meneja masoka la hissa  Patric Mususa,
akitoa taarifa ya wiki  juu ya soko hilo jijini Dar es Salaam













Idadi  ya mauzo katika soko la hissa Dar es salaam (DC) imeshuka kutoka bilioni 106 kwa wiki iliyopita hadi kufikia bilioni 2.5 kwa wiki hii.
             
Akizungumza na wingu la habari jijini Dar es salaam Meneja wa soko hilo Patric Mususa alisema kuwa katika soko hilo pia idadi ya hissa zilizonunuliwa na kuuzwa imeshuka kutoka milioni 8 hadi kufukia milioni 1.4 kwa wiki hii .

Alisema kuwa Kampuni tatu zinazoongoza katika soko hissa zake  kununuliwa na kuuzwa ni  CRDB BAKI, TBL, TCC,  kwani CRDB BAKI inaongeza kwa 90%, wakati TBL ikiwa na 5.8% uku kampuni  TCC ikiwa na asilimia 1.17.

Mususa amebainisha kuwa  mtaji katika soko hilo  imepungua kwa wastani kutoka tirioni 22.5 hadi tirioni 22.2,uku idadi ya mtaji wa kamupuni za ndani ikishuka kutoka tirioni 9.8 hadi 9.7.

Hata hivyo amezitaja Kampuni tatu zinazongoza hissa zake katika bei ni pamoja na Uchumi supermekert ikiwa na asilimia nne , kenya airway asilimia nne uku kampuni ya T way gases ikiwa na asilimia 1.3.

Sanjali na hayo alisema kuwa Kiashiria cha soko upande wa kibeki na fedha imeshuka kwa nukta 34 kikiwa kimechangiwa kwa kiasi kikubwa kushuka kwa mauzo katika kampuni ya CRDB na NMB, na katika sekta ya viwanda pia kimeshuka kwa nukta nne ikiwa imechangiwa kwa kushuka kwa mauzo katika kampuni ya TBL na Twiga cement.

‘’Kwa ujumla kiashiria cha soko kimeshuka kwa wastani ya nukta 16 ingawa soko linaoneka kuwa katika kiwango kizuri  licha ya kushuka kwa asimilima 98 kwa wiki hii, kwani kushuka uko kumechangiwa na Serikali wiki iliyopita kuja kununua na kuuza hissa yake ambazo waliwekeza muda mrefu’’ alisema.


Hata hivyo amebainisha kuwa katika upande wa kununua na kuuza hissa kwa njia ya simu wameendelea kupata mwitigio mzuri na kuwataka watu wengine waendeele kujiunga na huduma hiyo kwa kupiga namba *150*36# ambayo inayojulikana kwa jina DS MOBILE TRADE kwani mpaka sasa  wameongezeka watu kutoka 600 hadi kufukia watu 700 katika huduma hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here