![]() |
| Baadhi ya wanamgambo wa Syria |
Imebainika kwamba baadhi wa
wanamgambo wa Syria waliopewa mafunzo ya kijeshi na Marekani wametoa silaha zao
na kuwapa kundi la al-Nusra, lenye mafungamano na kundi la Al Qaeda.
Msemaji mkuu wa jeshi la Marekani alikiri kwamba wanamgambo hao
walisalimisha magari sita pamoja na silaha kwa kundi hilo mapema wiki hii.
Kundi hilo ni la pili kupewa mafunzo hayo ya kijeshi na wizara
ya ulinzi ya Marekani Pentagon na ni sehemu ya jumla ya wapiganaji 70.
Kundi la mwanzo kupewa mafunzo hayo lilivamiwa na wapiganaji wa
kundi la al-Nusra mara tu lilipoingia Syria mwezi Julai, na kuzusha wito wa
kufutwa kwa mafunzo hayo.

No comments:
Post a Comment