UJERUMANI YAENDELEA KUTIMIZA WAJIBU WAO KWA KUTOA MISAADA YA KIMAENDELEO. - WINGU LA HABARI- ONLINE

Breaking

TANGAZO

TANGAZO
Sugar free

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Saturday, September 26, 2015

UJERUMANI YAENDELEA KUTIMIZA WAJIBU WAO KWA KUTOA MISAADA YA KIMAENDELEO.

Kansela wa ujerumani Angela Merkel  akichangia jambo mjini New  york.







Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ameahidi kuwa Ujerumanin itatimiza wajibu wake wa kutenga asilimia 0.7 ya pato kwa ajili ya  kuendeleza kufadhili maendeleo katika maeno mbalimbali.
Akizungumza katika hadhara Kuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York nchini Marekani jana, Merkel amehimiza nchi nyengine kutekeleza wajibu wao ili watu wote duniani waweze kuishi maisha ya heshima.
Merkel aliongeza kuwa ni muhimu nchi zilizoendelea kiviwanda, zitimize ahadi zao kama  Ujerumani inavyoendelea kuchangia  dola bilioni 100 kwa nchi zinazoendelea kuzisaidida kuhifadhi mazingira kuanzia mwaka 2020.
Merkel amesema kwa njia hiyo  wataweza kujenga Imani na kuleta maendeleo kwa ujumla, Merkel pia alizumgumzia suala la wahamiaji barani Ulaya na kusema maelfu ya wahamiaji wanakimbia ugaidi na vurugu katika nchi zao.
Aliongeza kuwa lazima dunia ikabiliane na sababu zinazopelekea uhamiaji  baada ya kumalizika kwa mkutano huwo wa siku tatu, viongozi wakuu wa dunia wataanza mkutano mwengine Jumatatu ambapo watazungumzia   suala la uhamiaji barani Ulaya pamoja na vita vinavyoendelea nchini Syria.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here