![]() |
| Wachezaji wa Wekundu wa msimbazi Simba Sport Klabu. |
Zikiwa
zimebaki masaa machache kushuudia miamba ya soka hapa nchini simba na yanga
,ukiangalia katika michezo iliyopita Kocha
Muingereza wa Simba SC, Dylan Kerr hakuwa na wachezaji wake wote wa kikosi cha
kwanza kutokana na baadhi yao kuwa majeruhi, lakini ameweza kuiongoza timu
kucheza vizuri na kushinda.
Mchezo wa kwanza dhidi ya Afrikani Sports safu yake ya ulinzi ilimkosa Nahodha Msaidizi, Hassan Isahaka, viungo Jonas Mkude, Abdi Banda na mshambuliaji Ibrahim Hajib.Isihaka na Hajib walipona na kucheza mchezo wa pili, wakati mchezo wa tatu aliwakosa beki mwingine tegemeo wa kati, Juuko Murushid na mshambuliaji mkongwe Mussa Hassan Mgosi.
Wachezaji wote hao wamefanya mazoezi katika kambi ya Unguja na wako fiti kuelekea mchezo wa leo- maana yake Kerr ana wigo mpana wa wachezaji kwa ajili ya mchezo dhidi ya Yanga Sc hii leo.
Ambapo kikosi ambapo atakitumia leo ni pamoja
na Peter Manyika; Hassan Kessy, Mohammed
Hussein ‘Tshabalala’, Juuko Murushid, Hassan Isihaka, Justice Majabvi, Simon
Sserunkuma, Said Ndemla, Ibrahim Hajib, Hamisi Kiiza na Mussa Hassan Mgosi, kinachoweza
kuanza leo.
Lakini bado
Kerr anaweza kuamua kutumia viungo watatu na kupunguza mshambuliaji mmoja.
Tutaona muda ukifika.

Mshambuliaji wa simba Mussa Hassan Mgosi
akiwa katika ubora wake

akiwa katika ubora wake
Na Kocha Mholanzi wa Yanga SC, Hans van der Pluijm amekuwa katika wakati mzuri mwanzoni mwa Ligi Kuu, kwani hana majeruhi na amekuwa akipanga vikosi vyake atakavyo katika mechi zake za awali.
Hakuwa na mabadiliko kutoka kikosi cha ushindi wa mechi ya kwanza, ya pili hadi ya tatu na sasa mashabiki wa Yanga SC wamekwishaijua kikosi cha kwanza cha mwaka huu.
![]() |
Mchezaji wa yanga Amissi Tambwe |
kikosi hicho ni pamoja Ally Mustafa ‘Barthez’, Mbuyu Twite, Mwinyi Mngwali, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kelvin Yondan, Thabani Kamusoko, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Donald Ngoma, Amissi Tambwe na Godfrey Mwashiuya au Deus Kaseke.
Lakini leo
kunaweza kukawa na mabadiliko katika safu ya ulinzi, kutokana na taarifa za
Nahodha Cannavaro kuumia mazoezini kisiwani Pemba hivyo Kuna wasiwasi pia, Niyonzima
anaweza kuanzia benchi.
Haitakuwa ajabu leo, Barthez akianza pamoja na Juma Abdul kulia, Mwinyi kushoto, wakati katikati atalindwa na Twite na Yondan. Kamusoko amecheza vizuri mechi zote za awali, lakini leo anaweza kusogezwa juu, ili chini acheze Said Juma ‘Makapu’.
![]() |
| Benchi zima la ufundi likiongozwa Hans van der Pluijm. |
Kuna uwezekano pia Yanga SC ikaanza na viungo watatu, Salum Telela akiongezeka na kupunguza idadi ya mawinga, kwa sababu Simba SC ni timu yenye mtaji mzuri wa viungo.
Wachezaji wengi wamekuwa wakitajwa wiki yote hii kuelekea pambano la watani, kwa upande wa Simba SC, Hamisi Kiiza ‘Diego’ ndiye ameonekana kama mtaji mkubwa.
Lakini ukweli ni kwamba mtu hatari zaidi kwenye kikosi cha Simba SC kuelekea mchezo wa leo ni Mussa Hassan Mgosi, mchezaji mwenye uzoefu wa mechi za watani wa jadi kwa miaka 10 sasa.
Kama mchezaji, Mgosi ni fundi, hodari na mzoefu ambaye anawajua vizuri mabeki wa Yanga SC. Na zaidi Mgosi wa sasa si yule wa miaka mitatu iliyopita aliyekuwa anapenda kufunga mwenyewe tu- hapana huyu wa sasa anawatengenezea zaidi nafasi wengine.
Kiiza, Hajib na hata Awadh Juma wote, yeyote anaweza kutumbukiza mpira kwenye nyavu za Yanga SC, lakini mchezaji ambaye anatarajiwa kuwa na mvuto zaidi leo uwanjani kwa Simba SC, ni Mgosi.
AMISI JOSELYN TAMBWEM
ashabiki wa Yanga SC wameweka turufu zao zaidi kwa Donald Ngoma- kweli Mzimbabwe huyo ni hatari na anaweza kuwa tabu sana kwa Simba SC jioni ya leo.
Lakini mtu hatari zaidi kwa Simba SC leo ni Mrundi Amissi Joselyn Tambwe, ambaye hapana shaka kocha Hans van der Pluijm atamuanzisha kwa sababu anajua umuhimu wake awapo uwanjani.
Tambwe wa msimu huu, amekuwa anacheza kwa kuwafikiria kwanza wenzake kufunga na ndiye anaongoza hadi sasa kutoa pasi za mabao, lakini pia naye anafunga.
Tambwe amekutana na misukosuko mingi ya mabeki wa Tanzania na anawajua vizuri- isitoshe hao wa Simba SC amecheza nao anawajua kivitendo na maneno. Hakuna mtu wa kumtisha katika safu ya ulinzi ya Simba SC.
Uchezaji wa Tambwe umebadilika kwa kiasi kikubwa kutoka alivyokuwa Simba SC, na akiwa katika msimu wake wa pili Jangwani, tayari Mrundi huyo anajisikia yuko nyumbani.
YANGA MTEJA KWA SIMBA



No comments:
Post a Comment