Wekundu wa
msimbazi Simba Sport klabu pamoja
na watoto wa jangwani Yanga SC wote wanarejea leo jijini Dar es Salaam kutoka
kwenye kambi zao visiwani Zanzibar kwa ajiri ya pambano la ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara unaotarajia kupigwa
kesho katika dimba la taifa.
Miamba hiyo ya soka wanatarajiwa kuminyana kesho majira ya saa 10 jioni kwa saa za afrika mashariki , na katika maandalizi ya mchezo huo Yanga SC ilikuwa imeweka kambi kisiwani Pemba wakati mahasimu wao, Simba SC walikuwa Unguja kwa wiki yote hii kujiandaa vyema na mchezo huo.
Hivyo kuelekea mchezo huo hakuna majeruhi wa kutisha katika kambi zote mbili na makocha wote, Muingereza Dylan Kerr wa Simba SC na Hans van der Pluijm wa Yanga SC wemebainisha kuwa maandalizi yamekwenda vizuri na kila mmoja amejinadi kuondoka na alama tatu muhimu.
Sanjali na hayo Mchezo huo unatarajiwa kuchezeshwa na refa mwenye beji ya Shirikisho la Soka Kimataifa (FIFA), Israel Mujuni Nkongo wa Dar es salaam, atakayesaidiwa na Josephat Bulali wa Tanga, Ferdinand Chacha wa Mwanza, wakati mezani atakuwapo Soud Lila pia wa Dar es Salaam na Kamisaa atakuwa Charles Mchau kutoka Kilimanjaro.
katika michezo yao waliocheza hapo awali watani hao wa jadi wote walifanya vizuri baada ya kushinda medhi zao zote tatu za awali, Yanga ikizifunga 2-0 Coastal Union, 3-1 Prisons na 4-1 JKT Ruvu, wakati Simba ilizifunga 1-0 African Sports, 2-0 Mgambo JKT na 3-1 Kagera Sugar.
Mechi nyingine za Ligi Kuu ya Vodacom tanazania bara zitakazo pigwa kesho ni pamoja na Coastal Union dhidi ya Mwadui FC katika Uwanja wa Mkwakwani mijini Tanga.
Prisons na Mgambo JKT Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, JKT Ruvu
na Stand United Uwanja wa Karume, Dar es salaam, Mtibwa Sugar na Majimjaji ya
Songea Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro , Kagera Sugar na Toto Africans
Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
Ligi hiyo itaendelea kutimbua vumbi keshokutwa kwa michezo miwili, kati ya Azam FC na Mbeya City Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam na African Sports na Ndanda FC Uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga.

No comments:
Post a Comment