Raia mmoja wa Mali Ahmad Al Mahdi
Al Faqi, amefikishwa mbele ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu mjini the
Hague kwa madai ya kuhusika na uharibifu wa majengo ya kihistoria katika mji wa
Timbuktu.
Al Faqi alisalimu amri nchini Niger wiki moja iliyopita baada ya
kutolewa hati ya kukamatwa kwake.
Waendesha mashitaka wanamtuhumu Al Faqi kuwa ni mwanachama wa
kundi la Ansar Dine, la Waislamu wa itikadi kali ambalo limeshikilia eneo kubwa
la kaskazini mwa Mali tangu mwaka 2012.
Kundi hilo liliharibu majengo kadhaa ya kidini katika mji huwo
wa kihistoria, ikiwa ni pamoja na makaburi ya mashekhe wakubwa wa dini ya
Kiislamu
No comments:
Post a Comment