![]() |
| Mshambulizaji wa yanga Malimi Busungu akishangilia baada ya kuifungia timu yake goli. |
Watoto wa
jangwani Yanga wameibuka kidedea dhidi ya mnyamba Simba katika mchezo wa ligi ya Vodacom Tanzania bara baada ya kushinda
mabao mawili kwa bila katika mchezo uliopigwa leo katika dimba la taifa jijini dar
es salaam.
Katika mchezo
mshambuliaji Malimi Busungu ndiye amekuwa shujaa baada ya kutoa pasi ya bao na
kuifungia Yanga SC bao moja na kuibuka
na ushindi wa 2-0 dhidi ya mahasimu wao wa jadi, Simba SC .
Malimi aliyesajiliwa kutoka Mgambo JKT ya Tanga msimu huu, alimpa pasi Amissi Joselyn Tambwe kufunga baada ya kutokea benchi kipindi cha kwanza- kabla ya yeye mwenyewe kufunga la pili kipindi cha pili.
Mchezo huo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uliochezeshwa na refa wa FIFA, Israel Nkongo, hadi mapumziko, Yanga SC walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililofungwa na mshambuliaji Mrundi, Tambwe.
|
|
Tambwe
alifunga bao hilo dakika ya 44 kwa ustadi mkubwa, akigeuka baada ya pasi ya
Malimi Busungu aliyepokea krosi ya Haruna Niyonzima na kumchambua kipa Peter
Manyika.
Pamoja na kumaliza dakika 45 za kwanza wakiwa wanaongoza, Yanga SC hawakucheza vizuri kipindi cha kwanza na walikoswa mabao mawili ya wazi.
Simba SC walitawala mchezo kipindi cha kwanza na kuwafanya Yanga SC wapoteane kabisa uwanjani, kiasi cha kucheza kwa kujihami muda mrefu zaidi.
Dakika ya kwanza tu, Mwinyi Kazimoto alitia krosi maridadi, lakini mshambuliaji Hamisi Kiiza ‘Diego’ akachelewa na kipa Ally Mustafa ‘Barthez’ akadaka.
Beki Mkongo wa Yanga SC, Mbuyu Twite alifanya kazi nzuri dakika ya tano, baada ya kuokoa krosi nzuri ya beki wa kulia wa Simba SC, Hassan Kessy.
Dakika ya tisa, Nahodha wa Simba SC, Mussa Hassan Mgosi alishindwa kumalizia kazi nzuri ya kiungo Mwinyi Kazimoto na dakika ya 24 Kiiza alifumua shuti kali baada ya pasi ya Said Ndemla na Nahodha wa Yanga SC, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ akaokoa.
Shambulizi la kwanza la maana la Yanga SC lilikuja dakika ya 41, baada ya Tambwe kupiga shuti lililokwenda nje akiwa kwenye nafasi nzuri.
Kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm alimtoa mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu uliopita, Simon Msuva dakika ya 34 na kumuingiza Malimi Busungu aliyekwenda kuongeza uhai katika safu ya ushambuliaji ya Yanga SC.
Refa Nkongo alimuonyesha kadi
ya pili ya njano Mbuyu Twite dakika ya 90+2 kwa kujichelewesha kurusha mpira na
Simba SC walitumia dakika hizo za majeruhi kufanya shambulizi moja la maana
langoni mwa Yanga SC.
Ushindi huo, unaifanya Yanga SC ijinafasi kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ikitimiza pointi 12 baada ya mechi nne, wakati Simba SC inaanza kuporomoka.
Ushindi huo, unaifanya Yanga SC ijinafasi kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ikitimiza pointi 12 baada ya mechi nne, wakati Simba SC inaanza kuporomoka.
Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Mbuyu Twite, Mwinyi Kazimoto, Kevin Yondan, Thabani Kamusoko, Simon Msuva/Malimi Busungu dk34, Salum Telela/Said Juma ‘Makapu’ dk82, Amissi Tambwe/Deus Kaseke dk87, Donald Ngoma na Haruna Niyonzima.
Simba SC;Peter Manyika, Hassan Kessy/Pape Abdoulaye N’daw dk84, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Hassan Isihaka, Juuko Murushid, Justice Majabvi, Awadh Juma, Said Ndemla, Hamisi Kiiza, Mwinyi Kazimoto na Mussa Hassan Mgosi/Ibrahim Hajib dk62.

No comments:
Post a Comment