Shirikisho la kabumbu TFF leo
imeweka bayana viingilio vya mchezo wa
watani wa jadi Simba na Yang katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara unaotarajiwa
kuchezwa Jumamosi katika dimba la Taifa
jijini Dar es salaam.
Katika mchezo huo kiingilio cha
chini kitakua ni shilingi elfu saba (7,000) uku kiingilio cha juu kitakua ni
shilingi Elfu Thelathini (30,000) kwa viti vya VIP A, Elfu Ishirini (20,000)
kwa viti vya VIP B & C, huku kiingilio cha shilingi Elfu Saba (7,000)
kikiwa ni kwa viti vyenye rangi ya Blu, Kijani na Orange.
Hivyo tiketi za mchezo hou zitaanza kuuzwa siku ya Ijumaa kuanzia saa 2 kamili asubuhi katika vituo vifuatavyo, Karume – Ofisi za TFF, Buguruni – Oilcom, Dar Live – Mbagala, Uwanja wa Taifa, Luther House – Posta, Ferry – Kivukoni, Mnazi Mmoja, Ubungo – Oilcom na Makumbusho – Standi ya mabasi ya daladala.
Mchezo wa SIMBA NA YANGA utachezeshwa na mwamuzi wa kimataifa mwenye beji ya FIFA, Israel Nkongo kutoka jijini Dar es salaam akisaidiwa na Josephat Bulali kutokaTanga, Ferdinand Chacha wa Mwanza , mwamuzi wa akiba Soud Lila wa Dsm wakati kamisaa wa mchezo huo atakua Charles Mchau kutoka Kilimanjaro.
Michezo mingine ya Ligi Kuu ya Vodacom siku hiyo ya Jumamosi itakua ni kati ya wagosi wa kaya Coastal Union dhidi ya wachimba migodi Mwadui FC katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, Maafande wa jeshi la Magereza Tanzania Prisons watawakaribisha maafande wa Mgambo Shooting katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Uku Maafande wa JKT Ruvu watakuwa wenyeji wa Stand United katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam, wakati wakata miwa wa Turiani Mtibwa Sugar watawakaribisha Majimjaji ya Songea katika uwanja wa Manungu mkoani morogoro, Kagera Sugar watakuwa wenyeji wa Toto Africans katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
na siku ya Jumapili kutakuwa na michezo miwili ambapo waoka mikate wa Azam FC watawakaribisha Mbeya City katika uwanja wa Chamazi Complex, huku African Sports wakiwa wenyeji wa Ndanda FC kwenye uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
No comments:
Post a Comment