Timu ya taifa ya Wanawake ya mpira wa miguu Tanzania,
TWIGA STARS inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Taifa ya Wanawake ya Malawi
unaotarajiwa kupigwa 24 Oktoba mwaka
huu nchini Malawi.Akizungumzia mchezo huo wa kirafiki Msemaji wa Shirikisho la mpira miguu TFF Baraka Kizibuto alisema kuwa mchezo wa Twiga Stars dhidi ya Malawi itachezwa jijini Lilongwe baada kupata mwaliko wa chama cha soka nchini Malawi (FAM) kuialika Twiga Stars kwenda nchini Malawi kwa ajili ya mchezo huo.
Aidha amebainisha kuwa Mchezo huo wa kirafiki watatumia kama sehemu ya maandalizi ya vikosi vya timu zote mbili za Wanawake Tanzania na Malawi kwa ajili ya michuano mbalimbali .
Sanjali na hayo Mwenyekiti wa
Chama cha Soka ya Wanawake Tanzania (TWFA), Amina Karuma anatarajiwa kuhudhuria
kongamano la viongozi wa soka la wanawake duniania litakalofanyika Zurich
nchini Uswisi Septemba 28 hadi 02 Oktoba
mwaka huu.
Kongamano hilo linashirkisha viongozi 35 wanawake wa mpira wa miguu kutoka semehu mbalimbali duniani ikiwa ni muendelezo wa kongamano liliofanyika mwezi Machi mwaka huu nchini Canada wakati wa fainali za kombe la Dunia la Wanawake.
No comments:
Post a Comment