WANAWAKE TUCTA WAUNGANA KUPINGA UNYANYASAJI. - WINGU LA HABARI- ONLINE

Breaking

TANGAZO

TANGAZO
Sugar free

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Wednesday, March 7, 2018

WANAWAKE TUCTA WAUNGANA KUPINGA UNYANYASAJI.


Mwenyekiti wa Kamati ya Wanawake Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Neema Luganda akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.

WINGU LA HABARI
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM.
Wanawake nchini wametakiwa kuwa na ushirikiano ili kukemea mila zilizopitwa na wakati ambazo zimeonekana zinaendelea kukandamiza haki na unyanyasaji katika maeneo mbalimbali katika jamii.

Akizungumza katika kongamano la Wanawake, Mwenyekiti wa Kamati ya wanawake kutoka Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Neema Luganda, amesema kuwa wanawake wanapaswa kuwa na ushirikiano ili kuondoa unyanyasaji katika maeneo yao ya kazi.

Luganda amesema ushirikiano ni jambo la muhimu ambalo linaweza kutokomeza unyanyasaji kwa wanawake katika maeneo mbalimbali katika jamii.

“Kwa sasa unyanyasaji kwa wanawake umepungua na kuwa tofauti na miaka ya nyuma” amesema Luganda.

Luganda ameeleza kuwa takwimu zinaonyesha unyanyasaji kwa sasa umepungua…lakini wanawake wanatakiwa kuwa na umoja ili kuhakikisha wanabaki katika mazingira mazuri mahali popote.

Kwa upande wake Katibu wa TUCTA Dk. Yahaya Msigwa, amesema kuwa ili kuondokana na unyanyasaji wanawake wanatakiwa kukimea mila 
zilizopitwa na wakati ambazo zinaendelea kukandamiza haki ya mwanamke.

Dk Msigwa amesema kuwa wanawake ni wengi hapa nchini tofauti na wanaume, hivyo wanatakiwa kuwa pamoja jambo ambalo litasaidia kupigania maamuzi katika kutafuta haki zao.

“Wanawake wasikate tamaa kwani jambo rahisi kwao ni kupigania maamuzi ya kupiga unyanyasaji katika maeneo mbalimbali katika jamii” amesema Dk. Msigwa.

TUCTA leo wamefanya kongamano la siku ya wanawake duniani wakiwa na lengo la kumkumbusha mwanamke kuhusu usawa pamoja na kupinga unyanyasaji katika maeneo mbalimbali katika jamii.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here