KAMATI YA MKUU WA MKOA DAR WAKUTANA, SEKTA YA AFYA BADO CHANGAMOTO - WINGU LA HABARI- ONLINE

Breaking

TANGAZO

TANGAZO
Sugar free

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Wednesday, March 7, 2018

KAMATI YA MKUU WA MKOA DAR WAKUTANA, SEKTA YA AFYA BADO CHANGAMOTO

 Viongozi wa vyama vya siasa, wabunge, wajumbe wa kamati za ulinzi na Usalama, Wakuu wa Wilaya,  Wakurugenzi wa halmashauri, viongozi wa dini,  wakuu wa taasisi pamoja  watendaji mbalimbali wa sekretarieti ya mkoa na halmashauri wakiwa katika ufunguzi wa kikao cha kamati ya ushauri ya Mkoa kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam.



WINGU LA HABARI
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Hospitali za Mkoa wa Dar es Salaam bado kunaupungufu wa vitanda vya kulala wagonjwa hali inasababisha baadhi ya wagonjwa kulala chini.

Akizungumza katika ufunguzi wa kikao cha kamati ya ushauri ya Mkoa Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema, amesema kuwa katika hospitali za mkoa wa Dar es Salaam kuna msongamano wa wagonjwa. 

Amesema kuwa uwezo wa kulazwa wagonjwa katika hospitali za Mkoa wa Dar es Salaam ni vitanda 300 kwa kila hospitali, huku hali halisi za hospitali hizo zinalaza wagonjwa 450 hadi 500 kwa siku na kusababisha wagonjwa wengine kulala  chini.

Mjema ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda, amesema kuwa kuna idadi kubwa ya akina mama wanaojifungua kwa siku katika vituo vya huduma ya afya kutokana kuna wazazi 100 hadi 120 wapo katika hospitali za rufaa za mkoa.

“Hali hii inasababisha wazazi kulala chini na kupewa ruhusa kati ya saa 3 hadi 4 badala ya kukaa saa 48 badala ya kujifungua kama inavyoshauriwa na wataalam wa afya” amesema Mjema.

Mjema amefafanua kuwa pamoja na msongamano huo, bajeti ya huduma ya afya inayotolewa kwa mkoa wa Dar es Salaam haiendani na matumizi halisi kwani wananchi ni wengi.

Hata hivyo amebainisha kuwa licha ya changamoto hizo, serikali imeendelea na jitihada za kuboresha huduma za afya ikiwemo utoaji wa simu katika vituo 22 kwa ajili ya kuboresha huduma za rufaa ya mama na mtoto pamoja na hositali ya Taifa ya Muhimbili.

Ameeleza kuwa wamefanikiwa kujenga wodi ya wachanga na wazizi katika hospitali za rufaa za mkoa wa Amana, Temeke, Mwananyamala chini ya ufadhili wa Camel Oil pamoja na ujenzi wa jengo lenye gorofa 3 ambalo lipo katika hospitali ya Amana.

“Pia kuna ujenzi wa chumba cha upasuaji maalum kwa ajili ya wakinamama, wajawazito katika hospitali ya rufaa ya mwananyamala chini ya ufadhili wa GSM ambapo umeanza kutumika” amesema Mjema.

Katika hatua nyengine Mhe. Mjema amesikitishwa na vitendo vya ujenzi holela, uchafuzi wa mazingira, ongezeko la ombaomba pamoja na uwepo wa watu wasiokuwa  na shughuli maalum.

Katika ufunguzi wa kikao hicho, viongozi mbalimbali waliudhuria wakiwemo viongozi wa vyama vya siasa, wabunge, wajumbe wa kamati za ulinzi na Usalama, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa halmashauri, viongozi wa dini,  wakuu wa taasisi pamoja na watendaji wa sekretarieti ya mkoa na halmashauri

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here