Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda aliye vaakoti akiwa ameambatana na mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva na viongozi na maafisa wengi wa Wilayahiyo katika kukagua miradi.
WINGU LA HABARI
NaJohn Luhende.
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amempa majuma mawili Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke kupata eneo la kujenga shule ya msigi katika eneo la Mbagala Mbande ili kupunguza msongamano wa wanafunzi katika shule ya msingi Mbande .
Mhe. Makonda ameya sema hayoleo wakati wa ziara yake wilayani Temeke kukagua mpango mkati wa wilaya hiyo katika ujenzi wa shule na miradi mbalimbali ya maendeleo ambapoa amtembele Shule ya msingi Maji matitu ,ujenzi wa Zahanati ya Maji matitu ,Mradi wa maji wa DAWASCO Maji matitu na shule ya msingi Mbande ,na kushuhudia ongezeko la wanafunzi katika shule hizo.
Aidha amewataka watumishi wa serikali katika Idara mbalimbali kuhakikisha wanaitumia vizuri fedha zilizotengwa katika bajeti ili kutekeleza miradai ya maendeleo wilayani humo hususa ni katika secta ya elimu ambapo baada ya kutangazwa elimu bure uandikishaji wa wanafunzi umeongezeka maradufu hali iliyopelekea wanafunzi nwengi kurundikana Madarasani.
,, Nataka kila mtumishi katika idara awe mtu wa kutatua changamoto za wananchi na si mtu wa kutengeneza migogoro katika idara yako kama unaona pesa ulizo tengewa katika bajeti mbane mkurugenzi ili uweze kutimiza malengo na miradi ya idara yako sikyo kukaa ofisini na kusubiri tu,, Alisema
Kwa upande wa wazazi amewataka kuwa peleka watoto wa shuleni kupata Elimu ambayo kwa inatolewa bure huku akiwataka kuto wabagua watoto wa kike kwa kutegemea kuwa wataolea bali wawahesabu sawa na watoto wa kiume kwa kuwa wote nisawa , amesema kwa elimu ni ukombozi wa familia masikini na kuwa taka kuitumia fursa hiyo kuwaelimisha watoto hao ili kukomboa familia zao na kulisaidia Taifa.
Akitoa taarifa kwa mkuu wa mkoa kaimu Afisa Elimu msingi wilaya ya Temeke Slyvia Mutasingwa , Amesema kumekuwa na ongezeko la wanafunzi walioandikishwa mwaka huu darasa la kwanza mpaka leo asubuhi ni 1,130 huku lengo lilikuwa ni kuandikishwa wanafunzi 900 , wavulana 90 na wasichana 100 kitu ambacho ni zaidi ya maelengo.
Akitoa taarifa ya jumla ya Wilaya kielimu amesema halmashauri ya manispa hiyo inajumla ya wanafunzi 1,6625 , wavulana 81,718 wasichana 84,387 na Walimu 3,018 Wanaume 554 Wanawake 26,032 na kusema kuwa Manispaa hiyo inaupungufu wa vyumba vya Madarasa 1,565 huku mahitaji halisi yakiwa ni 3,718 na kufanya kuwa na upungufu vyumba 2149 na upungufu wa matundu vya vyoo 2,219 kwa Mbade pekee kuna maahitaji ya madarasa 153 madarasa yaliyopo ni 38 kunaupugufu wa madarasa 115, kwa upande wa matundundu ya choo kuna matundu 40 huku mahitaji halisi yakiwa ni 310, na kuna madawati 2298 yalipo ni 1990 kuna upungufu wa madawati 308.
Kwa upande wa ufaulu mwaka 2017 walifaulu 82% na kwa darasa la nne walifaulu 100% walifaulu.
Hatahiyo amesema Halmashauri imetenga bajet ya kununua eneo la Kujenga shule Kisewe na kuhakikisha maeneo yote ya shule yanapimwana na kuwekewa uzio.
No comments:
Post a Comment