Kutoka kulia ni Mtendaji Mkuu wa Atamizi ya Ujasiriamali kupita Teknohama (DTBi) George Mulamula akifatiwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bengi Issa.
WINGU LA HABARI
NA NOEL
RUKANUGA, DAR ES SALAAM.
Wajasiriamali
nchini wametakiwa kuchangamkia fursa za mpango wa kuwaendeleza kiuchumi katika
sekta mbalimbali ikiwemo kilimo, afya, mifugo pamojo, huduma za fedha kwa kutuma maombi ya wazo la biashara kupitia Baraza la Taifa la Uwezeshaji kiuchumi (NEEC), Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) pamoja na Atamizi ya Ujasiramali kupitia teknohama (DTBi).
Mpango
huo unafanywa na NEEC, COSTECH, DTBi kwa lengo la kuwasaidia wajasiriamali hapa nchini ili kuhakikisha wanapiga hatua katika uchumi na kufanisha Tanzania ya viwanda.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Katibu
Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bengi
Issa amesema
kuwa mpango huo una lengo la
kukuza sekta ya ujasiriamali katika kuhamasisha matumishi ya teknohama kama
nyenzo ya kuendeleza shughuli za uchumi.
Amesema
kuwa ili kupata fursa hiyo mjasiriamali anatakiwa kupeleka wazo la biashara la
ubunifu na kushindanishwa ili kupata washindi wenye mawazo mazuri ya biashara kwa kutumia ya teknohama.
“vigezo vya muombaji
lazima awe na wazo bunifu au biashara yenye kutatua changamoto katika jamii,
kuwa tayari kutumia teknolojia ya habari na mawasiliano katika biashara yake,
awe analipakodi za serikali na anatunza kumbukumbu za biashara pamoja na kuwa
mzaliwa wa Tanzania” amesema Issa.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Atamizi ya Ujasiriamali kupitia Teknohama (DTBi) George Mulamula, amesema kuwa kufanya hivyo itasaidia Tanzania kufika malengo ya kiuchumi wa viwanda.
Amesema kuwa
wajasiriamali watapata mitaji ambapo kutakuwa na mchakato wa uchambuzi wa maombi
utakaozingatia vigezo muhimu.
“Fomu za maombi ya fursa
za mpango huo zinapatikana kupitia tovuti ya Baraza www.uwezeshaji.go.tz
au ya DTBi ambayo ni www.teknohama.or.tz na kutumwa kwenye barua
pepe ya neec@uwezeshaji.go.tz”
amesema Mulamula.
Ameeleza kuwa kuwa zoezi
la utoaji wa fomu linatarajia kuanza februari 24 mwaka huu na kufika tamati
Machi 5 mwaka huu, huku mwezi April mwaka huu wanatarajia kuwatangaza washindi
na kuwawezesha.
Mulamula amefafanua kuwa
mpango huo ni kukuza sekta ya ujasiriamali katika kuhamasisha matumizi ya
teknolojia kama nyenzo ya kuendesha shughuli zao ili kuongeza tija.
Amesema awamu ya kwanza
ya mpango huu uatasaidia wajasiriamali wa kitanzania kupata fursa za mitaji na
mafunzo ambapo kutakuwa na mchakato kuwapata kwao.
No comments:
Post a Comment