MAUZO SOKO LA HISA YAMESHUKA - WINGU LA HABARI- ONLINE

Breaking

TANGAZO

TANGAZO
Sugar free

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Monday, February 26, 2018

MAUZO SOKO LA HISA YAMESHUKA

WINGU WA HABARI
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Afisa Masoko Mwandamizi wa Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE) Marry Kinabo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Mauzo ya Hisa (Turnover/ Liquidity)
Mauzo kwa wiki iliyoishia 23 Februari  2018 yalikuwa shilingi Bilioni 2.3 ikilinganishwa na mauzo ya shilingi bilioni 6.4 kwa wiki iliyoishia tarehe 16 Februari 2018.
Vile vile Idadi ya hisa zilizo uzwa na kununuliwa kwa wiki iliyoishia tarehe 23 Februari 2018 ni hisa milioni 3.3 ikilinganishwa na mauzo ya hisa ya milioni 11.6 kwa wiki iliyoishia tarehe 16 Februari 2018.
Kampuni zilizoongoza katika mauzo ya hisa kwa wiki iliyoishia tarehe 23 Februari  2018 ilikuwa kama ifuatavyo:
TBL……………………………………………30%
VODA …………………………………………25%
TPCC……………………………………………22%
Ukubwa Mtaji (Market Capitalization)
Ukubwa wa mtaji wa kampuni zote zilizoorodheshwa katika soko umepanda kwa Shilingi Bilioni 456 kutoka Shilingi Trilioni 22.4 wiki iliyopita hadi Shilingi Trilioni 22.95 wiki iliyoishia tarehe 23 Februari 2018. Ongezeko hilo limetokana na kupanda kwa bei za hisa zaKCB (8%), EABL (7%), DSE (1%) na SWISS (1%).

Ukubwa wa mtaji wa kampuni za ndani umepanda kwa Shilingi Bilioni 2 kutoka Trilioni 10.143 hadi kufika Shilingi Trilioni 10.145 wiki hii. Hii ni kutokana na kupanda kwa bei ya hisa ya SWISS (1%) na DSE (1%).
Viashiria (Indices)
Kiashiria cha kampuni zote zilizoorodheshwa katika soko yaani DSEI kimepanda kwa pointi 47 kutoka pointi 2,336 hadi 2,383 pointi hii ikiwa ni kutokana na kupanda kwa bei za hisa za Kenya Commercial Bank (KCB), East African Breweries Ltd (EABL), Swissport (SWISS) na Dar es Salaam Stock Exchange (DSE).  
Pia kishiria cha kampuni za ndani yaani TSI kimepanda kwa pointi 1 kutoka pointi 3,868 hadi pointi 3,869 kutokana na kupanda kwa bei za hisa za  Swissport (SWISS) na Dar es Salaam Stock Exchange (DSE).
Kiashiria cha sekta ya viwanda (IA) wiki hii imebaki kwenye wastani wa pointi 5286 kama wiki iliyopita
Kiashiria huduma za kibenki na kifedha (BI) wiki hii imepanda kwa poniti 1 kutoka pointi 2,608 kadi pointi 2,609 hii imechangiwa na kupanda kwa bei za hisa za DSE kwa asilimia 1% kutoka shilingi 1580 hadi 1600.
Kiashiria cha Sekta ya huduma za kibiashara (CS) wiki hii imepanda kwa pointi 2 kutoka pointi 2,462 hadi pointi 2,464 imechangiwa na kupanda kwa bei za hisa za SWISS kwa asilimia 1% kutoka shilingi 3500 hadi shillingi 3540.
 Hati Fungani (Bonds)
 Mauzo ya hati fungani katika wiki iliyoishia tarehe 23 Februari 2018 yalikuwa Shilingi bilioni 64 kutoka Shilingi Bilioni 8 wiki iliyopita ya 16 Februari 2018. 


Mauzo haya yalitokana na hatifungani kumi na sita (16) za serikali zenye jumla ya thamani ya Shilingi bilioni 68 kwa jumla ya gharama ya Shilingi bilioni 64.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here