Mama wa Mitindo na Mwanzilishi wa Lady In Red nchini Asya Idarous wa tatu kutoka kulia akizungumza na waandishi wa habari, wa kwanza kutoka kushoto ni Afisa wa Mipango wa Lady in Red Omary Rashid.
Emmanuel Joseph Kisosi wa kwanza kutoka (kulia ) ni Fashion Designer akizungumzia maandalizi yake kuelekea onyesho la 1 5 farewell lady in Red litakalofanyika februari 9 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
.................
WINGU
LA HABARI
NA NOEL
RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Mwanamitindo
mkogwe nchini Tanzania Asya Idarous ametangaza kustaafu kuandaa jukwaa la ‘Lady
in Red’ kutokana na kufanya kazi hiyo kwa muda mrefu pamoja na kuwapa fursa
vijana wa kitanzania kulianda jukwaa hilo.
Asya Idarous
Khamsini ni jukwaa la kwanza Tanzania lililoanza kupandisha wabubifu chipukizi,
lakini ameeleza kuwa bado ataendelea kuonyesha mitindo yake katika majukwaa ya
kualikwa katika mitindo yake ya stara.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Asya Idarous, amesema kuwa kuanzia
sasa hataweza kuandaa jukwaa la ‘lady in led’ na badala yake kazi hiyo amewapa
vijana ili waweze kuandaa.
Amesema
kwa muda mrefu amefanya kazi ya kuandaa jukwaa la ‘lady in red’ na kufanikiwa
kuinua vipaji vya wabunifu chipukizi ambapo awali ilikuwa vigumu kupata nafasi kwa
ajili ya kuonyesha vipaji vyao.
“Nimekuwa
kukiandaa jukwaa la ‘lady in red’ kwa muda wa miaka 15 mpaka sasa nilikuwa
nawachukua vijana wabunifu kutoka mtaani ili waweze kuonekana na kufanikiwa”amesema
Idarous.
Ameeleza
kuwa kazi ya mitindo ataendelea kuifanya kutokana ni kazi ambayo anaipenda pia inaniingizia
kipato.
Idaraus
amewashukuru wadau mbalimbali ikiwemo Balaza la Sanaa Taifa (BASATA) kwa kumpa
ushirikiano katika kipindi chote cha kufanikisha maandalizi ya jukwaa la Lady
in Red.
Kwa
upande wake Afisa Mipango wa Lady in Red 2018 Omary Rashid amesema kuwa licha mama
wa mitindo kustaafu wanamni wataendelea kuandaa jukwaa hilo na kupata mafanikio
makubwa.
Amesema
kuwa wataendelea kuwa naye ili kuhakikisha wanapata ushauri rafiki katika
kufikia masula mbalimbali ya kimaendeleo ambao wamekusudia kuyafanya.
“Wadau
mbalimbali wanatakiwa kuendelea kutupa ushirikiano katika nyanja mbalimbali ili
kuhakikisha tunapiga hatua kubwa katika sekta ya ubunifu” amesema Rashid.
Akizungumzia
maandalizi ya uonyesho la 15 ‘Farewell Lady in Red’ linatorajiwa kufanyika
februari 9 mwaka huu katika ukumbi wa King Solomo uliopo namanga jijini Dar es
Salaam.
Rashid
amesema kuwa washiriki wa onyesho hilo wamejiandaa vizuri, huku akiwataka wadau
wa sanaa kutoka sehemu mbalimbali kufika katika ukumbi huo kwa ajili ya kuona
kazi za wabunifu.
Rashid
amefafanua uonyesho hilo litaanza saa mbili usiku pamoja kufanya mnada wa
kuchangia free at last sober house Morogoro kwa ajili ya kuisaidia jamii.
Farewell
Lady in Red 2018 ni onyesho la 15 na onyesho la 216 kwa Tanzania kwa Mama wa
Mitindo Asya Idarous Khamini ambapo ni jukwaa la kwanza hapa nchini kupandisha
wabunifu chipukizi na wazoefu.
No comments:
Post a Comment