Mwanzilishi wa Chama
cha Wanamitindo Tanzania (FAT), Mustafa Hassanali (wa pili kutoka kulia) akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa chama hicho leo jijini Dar es Salaam
Katibu
Mtendaji Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Godfrey Ngereza akizindua chama FAT leo jijini Dar es Salaam.
Wanzilishi wa Chama cha FAT Asia Idarous (wa kwanza kutoka kushoto) akiongea na waandishi wa habari, wengine waliosimama ni wanamitindo mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja.
WINGU LA HABARI
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES
SALAAM.
Wanamitindo nchini wametakiwa
kujiunga katika chama chao jambo ambalo linaweza kuleta chachu ya maendeleo
katika kufanikisha Tanzania ya Viwanda kupitia ubunifu wao.
Akizungumza na waandishi wa
habari leo jijini Dar es salaam katika uzinduzi wa Chama cha Wanamitindo
Tanzania (FAT), Mustafa Hassanali amesema lengo la chama ni kuendeleza
maslahi ya sekta ya mitindo kwa kuwaunganisha na kugawana ujuzi, uzoefu na
rasilimali katika sekta hiyo.
“FAT pia imelenga kukuza na
kuimarisha sekta ya mitindo nchini. Sisi kama wabunifu tunaunga mkono juhudi za
rais Magufuli katika kuifanya nchi kuwa katika uchumi wa viwanda vya kati
ifikapo 2025 kwa kuongoza katika bidhaa za nguo na vitambaa zinazotoka
Tanzania,” amesema Hassanali.
Ameongeza sekta ya mitindo inakuwa kwa haraka huku wadau
wake wanakumbana na changamoto nyingi, lakini bado wanaendelea kutafuta mafanikio
kwa kuanzishwa chama hicho chenye nia ya kuimarisha uhusiano mzuri wa wafanyaji
kazi za mitindo.
Mama wa Mitindo na Mwanzilishi wa
Lady In Red nchini Asia Idarous, amesema chama hicho hakijaundwa kwa ajili ya
wabunifu tu bali hata kwa wadau wote wa sekta ya mitindo, majukwaa mbalimbali
ya mitindo, taasisi za mitindo, wanamitindo (models) na wanamitindo wanaopanga
mavazi (Stylish).
Asia Idarous amesema kuwa watu wote
wa sekta ya mitindo na majukwaa mbalimbali, taasisi za mitindo wapaswa kujiunga
katika chama hicho.
Idarous ameeleza kuwa wadau wengine katika chama
hicho ni wanamitindo wanaopanga muonekano wa mavazi (stylist), wapiga
picha wa mtindo, makampuni ya nguo, wazalishaji na wauzaji mavazi na
wanaojihusisha na kazi za mitindo na urembo.
Hata hivyo amewataka wafanyakazi katika sekta ya
mitindo hapa nchini kujiunga katika chama hicho ili kupaza sauti zao katika
kutafuta fursa mpya za mitindo pamoja na kutatua changamoto zinazowakabili
katika tasnia ya mitindo.
Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa
la Taifa (BASATA) Godfrey Ngereza, amesema kuwa ni hatua nzuri wanaofanya
wanamitindo kwani ni sehemu ya mafanikio katika kupiga hatua.
Amesema kuwa ni wakati umefika
wanamitindo kuwa na upmoja hasa katika kipindi hiki taifa lipo katika ujenzi wa
viwanda kwa ajili kufika uchumi wa kati.
“Wabunifu ni watu wa muhimu
katika kuhakikisha wanatumia ubunifu wao kwa ajili ya kufanikisha Tanzania ya
viwanda” amesema Ngereza.
Amefafanua kuwa chama cha
wanamitindo kwa sasa watafika mbali katika kufanikisha kazi zao na kufanya
vizuri ndani na nje ya Tanzania.
Hata hivyo Ngereza ameeleza
kuwa wataendelea na mipango ya kukufua vipaji vya watoto kuanzia ngazi ya shule
ya msingi hadi sekondari, kwani kufanya hivyo itasaidia kuleta chachu ya
maendeleo katika kukuza vipaji.
No comments:
Post a Comment