WINGU LA HABARI
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Baadhi ya magari ambayo yanapigwa mnada na TRA kupitia kampuni ya Udalali Yono Auction Mart.
Wateja wa magari wakifatilia kwa makini mnada wa magari
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kupitia Kampuni ya Udalali Yono
Auction Mart wameendelea kupiga mnada wa magari katika bandari ya Dar es Salaam
kwa ajili ya kukusanya kodi ambazo zinaitajika katika kufanikisha shughuli za
kimaendeleo.
Mnada huo mkubwa umefanyika leo baada ya magari kukaa muda
mrefu kwa kile kinachodaiwa wahusika kushindwa kuyalipia kodi na watu kuchangamkia
fursa kwa kujitotekeza kutoka mikoa mbalimbali na kufanikiwa kununua magari
hayo.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji Kampuni
ya Yono Auction Mart Scolastica
Kevela, amesema kuwa mnada umekwenda vizuri kutokana na idadi kubwa
ya wateja kununua magari kwa bei nzuri.
Ameeleza kuwa ununuzi wa magari umefanyika kwa asilimia
kubwa na wanaendelea kuwashukuru wateja ambao wamekuwa wakiunga juhudi za
serikali za kukusanya kodi kupitia mnada huo.
“Tunawaomba watanzania waendelee kuja pale wanaposikia Yono Auction
Mart wanafanya mnada kwa niaba ya TRA kwani kufanya hivyo tutalijenga taifa la
Tanzania” amesema Kevela.
Gari aina ya Benzi lililonunuliwa kwa sh miloni 15
Baadhi ya magari yanayopigwa mnada na TRA
Katika hatua nyengine amebainisha kuwa januari 25 na 27 mwaka
huu, katika bandari ya Dar es Salaam kutakuwa na mnada mwengine kubwa wa magari
ya aina mbalimbali.
Kevela ameeleza kuwa siku moja kabla ya mnada huo kuanzia saa
tatu asubuhi hadi saa 10 jioni katika eneo la bandari wateja wanapaswa kufika
kwa ajili ya kufanya ukaguzi wa magari hayo.
“Watu wasikatishwe tamaa kuwa mnada huu wa magari una bei
kubwa, kwani tumeshudia leo wateja wetu wakinunua magari kwa bei nafuu….tunawaomba
waendelee kuja ili serikali ikusanya kodi yake” amesema Kevela
Mkurugenzi Mtendaji Kampuni ya Yono Auction Mart Scolastica Kevela.
No comments:
Post a Comment