WINGU LA HABARINA NOEL RUKANUGA,DAR ES SALAAM Klabu ya Simba leo imemtambulisha kocha mpya Mfaransa Pierre Lechantre pamoja na kocha wa viungo Mtunisia Aymen Habib. Kocha mpya wa Simba Pierre Lechantre (katikati) akiwa ameshika jezzi ya simba (wakwanza kushoto) ni kaimu rais wa Simba, Salim Abdallah na wa mwisho kulia ni Meneja wa kocha huyo Joe Onegofro jijini Dar es salaam.
Akizungumza baada ya kusaini makubaliano ambayo hayakuwekwa wazi, kocha hiyo amesema atakuwepo kwa muda mrefu kwa kuwa klabu ina malengo ya muda mrefu kwa ajili ya kuwa bora barani Afrika.
“Nipo hapa kwa ajili ya ‘project’ ya muda mrefu ili kuhakikisha timu inakuwa bora, ninaweza kuwepo hapa kwa miaka mitatu au zaidi,” amesema Lechantre.
Amewetaka kwa sasa mashabiki na wapenzi wa mpira nchini kuweka pembeni wasifu wake na waangalie kazi ambayo amekuja kuifanya na kueleza kuwa mabadiliko katika timu yanaweza kuanza kuonekana baada ya miezi miwili.
Kwa upande wake msemaji wa Simba Haji Manara, amesema kocha huyo atasaidia pia katika maendeleo ya timu za vijana kwani klabu inamalengo makubwa.
Pia amewataka mashabiki wasimba kuwa na uvumilivu pale klabu inapofanya vibaya kwani hakuna anayependa kutokea jambo hilo. Kocha mpya wa simba Pierre Lechantre akibadilishana mkataba na kaimu rais wa simba Salim Abdallah baada ya kutiliana saini jijini Dar es Salaam.
Kaimu rais wa Simba Salim Abdallah akiwa ameshika jezi yenye jina la kocha wa viungo Aymen Habib.
No comments:
Post a Comment