Mfanyakajazi wa TRA, akimhudunia mteja katika
Kituo cha kuandikisha walipakodi eneo la Chanika.
Mamlaka ya Mapato Nchini
(TRA) imesema kuwa wanatarajia kusajili walipakodi wapya 1000,000 ambao
watalipa kodi Sh. Bilioni 1.5.
Akizungumza katika usajili
wa kituo cha kusajili wafanyabiashara wa dogo cha Chanika, Kamishna wa Kodi za
Ndani, Elijah Mwandumbya amesema kuwa kampeni ya kusajili wafanyabiashara wa
dogo ni endelevu.
Kamishna wa Kodi za Ndani, Elijah Mwandumbya, akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la Chanika.
Elijah amesema kuwa wananchi Wajitokeze kusajiliwa kadri kodi zinavyolipwa ndiyo zinafanya maendeleo ya nchi.
Amesema kuwa uhamasishaji wa ulipaji kodi na usajili utaendelea kwa kuweka vituo karibu na wafanyabiashara.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa elimu kwa mlipa kodi wa
Mamlaka hiyo Richard Kayombo amewataka wananchi wa naishi maeneo hayo
kujitokeza kwa wingi kwaajili ya kujiandikisha na kusema kuwa zoezi hilo
katika Kituo hicho Litadumu kwa muda wa juma moja.
"tukitoka Manispaa ya Ilala tuta elekea Temeke na baadaye
Tutaendelea kufungua vituo katika maeneo mbalimbali" alisema Kayombo.
Aidha Kayombo amesema, Mamlaka hiyo imeamua kuja na kampeni
hii baada ya kutambua kuwa kulikuwa na usumbufu kwa Wafanya biashara
kupata TIN namba, kutokana na umbali kutoka wakazi wa eneo hilo hadi
Vingunguti, na sasa wamesomea huduma hiyo na kwamba watakaoandukisha hawana
lazima kulipa kodi siku hiyo hiyo.
Pamoja na hayo amewatahadhalisha wananchi kutolaghaiwa na
matapeli kwani kazi hiyo inafanya na TRA yenyewe na hakuna wakala aliye pewa
kazi hiyo.
No comments:
Post a Comment