Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC Dk. Helen Kijo-Bisimba wa pili kutoka kushoto, akizungumzi na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Na Noel Rukanuga
Kituo cha Sheria na Haki za Binadam (LHRC), kinampango wa kutoa taarifa kwenye vyombo vya kimataifa vinavyohusika na uangalizi wa haki za binadamu kwa ajili ya kuomba msaada kutokana na kile kinachodaiwa hakuna uhuru wa kujieleza na maoni hapa nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC Dk. Helen Kijo-Bisimba amesema kuwa watatoa taarifa kwenye vyombo vya kimataifa ili waingilie kati suala la uhuru wa kujieleza hapa nchini.
Kauli hiyo ya Bisimba imekuja siku moja baada ya Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) kuvitoza vituo vitano vya televisheni faini ya sh. milioni 60 kutokana na makosa mbalimbali yaliyotokana na kuripoti taarifa ya tathmini ya uchaguzi mdogo wa madiwani iliyotolewana LHRC.
“Tumeshuhudia serikali kupitia TCRA ikitoa adhabu kwa vituo vitano vikubwa vya luninga ambavyo nia Azam TV, ITV, Channel 10, Str TV na EATV kwa kile kinachodaiwa kuwa ni ukiukwaji wa kanuni ya maudhui 2005 baada ya televisheni hizo kurusha habari kuhusu tathmini ya haki za binadamu katika uchaguzi mdogo wa madiwani uliofanyika Novemba 2017 iliyotolewa na LHRC,” amesema Dk. Kijo-Bisimba.
Ameongeza “LHRC imechukua hatua ya kutoa taarifa kwa vyombo vya kimataifa vinavyohusika na uangalizi wa haki za binadamu kuomba waingilie kati suala la uhuru wa kujieleza nchini,”
Dk. Kijo-Bisimba amesema kufuatia hatua hiyo ya TCRA, LHRC imechukua hatua ya kuwandikia barua TCRA kuwataka kufanya semina kwa kituo hicho na taasisi nyingine juu ya namna bora ya kuandaa maudhui.
Hata hivyo amefafanua kuwa wameanzisha harambee ya kuchangia gharama ya kuvisaidia vyombo vya habari vilivyokumbwa na adhabu pamoja na kuungana na wadau ambao wako tayari kwenda mahakamani kuomba tafsiri ya neno UCHOCEZI na baadhi ya vifungu vya kanuni ya maudhui hususani kifungu namba 8 katika mazingira ya utawala wa serikali dhidi ya raia.
Kwa mujibu wa kamati ya maudhui ya TCRA, vyombo hivyo vimetiwa hatiani kwa makosa matatu chini ya kifungu cha 5 na 6 vya kanuni za maudhui za mwaka 2005 na kupigwa faini kwa viwango tofauti pamoja na kuwekwa chini ya uangalizi kwa miezi sita.
No comments:
Post a Comment