WINGU LA HABARI
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani
Jafo akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo
Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya
Butiama Mkoani Mara baada ya kushidwa kusimamia vyema majukumu yake.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo amesema
kuwa Mkurugenzi huyo ni Solomon Ngiliule ambaye uteuzi wake umetenguliwa kuanzia
sasa.
Amefafanua kuwa baada ya kutenguliwa uteuzi
huo, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais- TAMISEMI anapaswa kuchukua hatua stahiki kwa Mweke Hazina aliyekuwepo wakati matumizi mabaya ya
fedha za serikali zinafanyika katika halmashauri hiyo.
“Katibu Mkuu anatakiwa kumchukulia hatua stahiki Mweka Hazina ambaye alikuwepo wakatika Mkurugenzi anafanya matumizi mabaya
ya fedha za serikali” amesema Mhe. Jafo.
Mhe. Jafo ameeleza kuwa kwa sasa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wanaendelea na uchunguzi ili kubaini kiasi gani cha fedha kilichotumia vibaya.
Hata hivyo amewataka watendaji wote walio chini ya Tawala za Mikoa
na Mamlaka za Serikali za Mitaa kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia kanuni za utumishi wa umma na kuhakikisha rasilimli
za umma na nchi zinatumika kwa mslahi ya wananchi.
Kutumbuliwa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Butiama Solomon Ngiliule kumetokana na ziara ya kikazi iliyofanywa na Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ambapo ilibainika
watendaji wa halmshauri wameshindwa kusimamia vyema maeneo yao kazi.
No comments:
Post a Comment