TANZANIA KUFAIDIKA NA BIASHARA YA MAGARI YANAYOTUMIA UMEME. - WINGU LA HABARI- ONLINE

Breaking

TANGAZO

TANGAZO
Sugar free

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Monday, January 22, 2018

TANZANIA KUFAIDIKA NA BIASHARA YA MAGARI YANAYOTUMIA UMEME.

WINGU LA HABARI
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM



Mradi wa Ngualla mine ambapo hadi sasa wametumia dola milioni 32 kwa ajili ya  kufanikisha  mradi  huo.
Meneja wa Biashara Kampuni ya PR NG Minerals Ismail Diwani akizungumza na waandishi  wa habari leo jijini Dar es Salaam

 Nyumba za Walimu zilizojengwa na PR NG  Minerals huko Ngwala. Nyumba hizi ni sehemu ya nyumba 9 za walimu zilizojengwa mpaka sasa katika vijiji vitatu vinavyozunguka mradi huo.

Picha ya gari inayotumia umeme.

Kampuni ya PR NG Minerals na Peak Resources zimezamilia kuleta mapinduzi katika biashara ya magari yanayotumia umeme baada ya kufanya utafiti hapa nchini wa kuanzisha mradi wa kuchakata madini ya Neodymium na Praseodymium (NdPr) yanayowezesha utengenezaji wa magari hayo.

Magari hayo yanayotumia umeme hujulikana kama ‘E- Mobility’ambapo utumia mota za umeme ambazo kwa kiasi kikubwa utumia sumaku za Neodymium na Praseodymium (NdPr) ambazo zinapatika hapa nchini Tanzania.

Kuanza kwa mradi wa ‘Ngualla Rate Earth Project’ uliopo Kata ya Ngwala Mkaoni Songwe utatoa fursa za ajira kwa watanzania zaidi ya 1,000 ambapo sawa na asilimia 98, huku serikali ikipata kodi ya Sh bil 25 kwa mwaka.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Afisa Mkuu wa Maendeleo Kampuni ya Peak Resources Lucas Stanfield, amesema kuwa ni habari njema kwa Tanzania kuwa na rasilimali za madini ya NdPr yenye ubora wa hali ya juu duniani.  

Amesema kuwa wazalishaji wa magari madogo na malori duniani wameanza kuhama kutoka katika kutengeza magari yanayotumia injini za petroli na dizeli na sasa wamebadilisha mfumo na kutengeza magari yanayotumia umeme.

Stanfield amesema kuwa mradi huo utadumu kwa miaka 31 kwani kufanya hivyo itasaidia Tanzania kuwa katika nafasi ya mzalishaji mkubwa wa madini ya NdPr tofauti na awali kwani ilikuwa nchi ya China.



Ameeleza kuwa PR NG Minerals imewekeza zaidi ya dola za kimarekani 320,000,000 katika utafiti wa NdPr na kuendeleza teknolojia inayotakiwa kwa kuchimba madini haya kutoka katika miamba.

“Hii si kama dhahabu ambapo kuna nji zilizokwisha jaribiwa na kuthibitishwa za kuchakata Ore” amesema Stanfield.

Anasema kuwa NdPr ni bidhaa ya kitaalamu ambapo ni makampuni machache tu yanao ujuzi wa kuchimba pamoja na kuisafisha oxide.

Amebainisha kuwa Kampuni ya PR NG imekamilisha upembuzi yakinifu na imethitisha kwamba inao uwezo wa wa kuchakata madini haya ya kipekee kutoka wilaya ya Ngualla Mkoani Sogwe.

“Hatua inayofuata kwa sasa ni kujadiliwa kwa ombi letu la leseni (SML), ambapo  liliwasilishwa mwezi August mwaka jana, ili tuweze kuendelea na ujenzi”amesema Stanfield.

Imeeleza kuwa ujenzi wa mgodi na mtambo wa kuchakata unakadiriwa kuwa dola za kimarekani milioni 200 na pia itahusisha ujenziwa miundombinu muhimu ikiwemo ukarakabati mkubwa wa barabara pamoja na kazi inayokadiriwa kugharimu dola za kimarekani milioni 22.

"Tumekuwa tukipata uungwaji mkono mkubwa kutoka kwa jamii zinazozunguka na mradi" amesema Stanfield.

Ameeleza kuwa programu za maendeleo zilizofanyika mpaka sasa katika eneo la mradi  ni pamoja na ujenzi wa madarasa na nyumba za walimu ambapo  ni seheme ya faida zitakazoletwa na mradi huu katika eneo hasa katika nyanja za kuboresha miundombinu na ajira kipindi watakapoanza kazi.


Mradi utakapoanza unatarajiwa kutoa ajira za moja kwa moja kwa zaidi ya watu 200 na ajira zaidi 1,000 zisizo zaa moja kwa moja. 

Hata hivyo Stanfield amesema kuwa mradi huo utatumia  umeme wa generator ambapo  kwa mwaka watatumia 42.3 MWh. 

 Kwa upande wake Meneja wa Biashara Kampuni ya PR NG Minerals, Ismail Diwani amesema kuwa  mwelekeo wa kuzalisha magari yanayotumia umeme yanatarajiwa kushika kadiri nchi zinavyoelekea katika malengo ya kupunguza matumizi ya mashine zinazotoa moshi.

Amesema kuwa nchini Ufaransa na Uingereza zimeazimia kuiga marufuku mauzo ya magari yanayotumia petroli na dizeli ifikapo mwaka 2040.

Diwani ameeleza kuwa wazalishaji wakubwa wa magari kama Volvo wamesema kuwa kuanzia mwaka 2019 aina zote za magari watakayoyatengeza yatakuwa yakitumia umeme zaidi.

Amesema kuwa kuongezeka kwa uzalishaji wa magari ya umeme kutaamaisha ongezeko kubwa la mahitaji ya NdPr na matarajio yakiwa ni ukuaji wa asilimia 100 kwa mwaka 2016 na 2025.

Muonekano wa maradi wa pili katika kufanikisha mfumo wa kuchakata madini  ya Neodymium na Praseodymium (NdPr).

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here