Wanafunzi wa Chuo Cha Taifa Cha Utalii wakiwa katika Maandamo ya Mahafali ya 15 yaliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Na Noel Rukanuga.
Uongozi wa Chuo Cha Taifa Cha Utalii umetakiwa kufungua
fursa za ajira kwa wahitimu kwa kuwa na miradi mbalimbali ikiwemo Hotel jambo
ambalo linaweza kuwasaidia wanafunzi kujifunza kwa vitendo na kuleta chachu
katika kuchochea Tanzania ya viwanda.
Akizungumza katika Mahafali ya 15 ya Chuo cha Taifa Cha Utalii,
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga ameema
kuwa Chuo kinatakiwa kuna miradi kama hotel jambo ambalo linaweza kuleta
maendeleo katika sekta ya utalii hapa nchini.
Mhe. Hasunga ambaye ni mgeni rasmi katika mahafali hayo, amesema
kuwa kuna mambo mengi ambayo yanapaswa kufanyiwa kazi na chuo ikiwemo kufanya
utafiti ili kuboresha taaluma.
“Lengo ni kupanua fursa katika sekta ya utalii hapa nchini
hivyo, chuo kinatakiwa kufanya tafiti ili kuleta tija katika nyanja mbalimbali
za kimaendeo” amesema Mhe. Hasunga.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga
Afisa Kaimu Mtendaji Mkuu Chuo Cha Utalii Taifa, Dk
Shogo Mlozi
Amefafanua kuwa katika kuboresha utalii hapa nchini Wizara
yake ipo katika hatua ya kubainisha utalii uliokuwepo katika mikoa zote hapa
nchini na kuzitangaza jambo ambalo litakuwa na manufaa katika kufika lengo.
Amesema kuwa kutokana na jitiada mbalimbali zinazofanywa na
serikali hadi kufika mwaka 2020 sekta ya utalii itakuwa inaingiza sh bilioni 4.
Katika hatua nyengine Mhe. Hasunga amewapongeza na
kuwatunuku vyeti wanafunzi zaidi ya 129 ambao wamemaliza masomo yao katika kozi
mbalimbali ngazi ya Astashahada, Stashahada katika chuo cha utalii.
Afisa Kaimu Mtendaji Mkuu Chuo Cha Utalii Taifa, Dk Shogo
Mlozi amesema kuwa licha ya changamoto kadha chuo kumefanikiwa kupinga hatua
katika nyanja mbalimbali.
Dk Mlozi amesema kuwa kwa sasa chuo kina Campus ya Bustani,
Temeke pamoja na Arusha ambapo wanafunzi wanaendelea kupata elimu.
Ameeleza kuwa kuna changamoto ya ukosefu wa vyumba vya
kujisomea katika Compus ya Temeke pamoja na ukosefu wa bajeti kwa ajili ya
kukamilisha shughuli mbalimbali za ofisi ikiwemo kufanya utafiti.
Amewataka wanafunzi hao kwenda kuwa kuwa mabolozi wazuri
jambo ambalo linaweza kuleta tija kwa taifa.
Hata hivyo wahitimu wameonekana kuwa na furaha na Kuwaiti kwenda
kufanya vizuri katika kulitumikia taifa kupitia elimu waliyopa katika chuo hicho.
Chuo cha Taifa Cha Utalii katika Compus ya Arusha na Bustani
zinatoa taaluma mbalimbali ikiwemo ‘Front Operations Skills, House Keeping and
Laundry Skills, Menu Planning, Menu costing and Pricing, Customer care and Team
Building in Service Industry pamoja na Food Preparation and Cooking Skills’.
No comments:
Post a Comment