BIDHAA YA SUGAR FREE YALETA MATUMAINI MAPYA KWA WAGONJWA WA KISUKARI. - WINGU LA HABARI- ONLINE

Breaking

TANGAZO

TANGAZO
Sugar free

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Saturday, December 16, 2017

BIDHAA YA SUGAR FREE YALETA MATUMAINI MAPYA KWA WAGONJWA WA KISUKARI.

 Meneja wa Masoko Kampuni ya ABACUS Pharma Jeremiah Bwana.
Na Noel Rukanuga.
Kampuni ya ABACUS Pharma imefanikiwa kuleta ahuweni kwa watu wenye matatizo ya kisukari hapa nchini baada ya kuzindua bidhaa ya ‘Free Sugar’ ambayo inawapa fursa watanznia wote kutumia bidhaa hiyo bila kupata madhara yoyote ya kiafya.

Sugar Free ni bidhaa mpya ya sukari ambayo inawapa fursa wagonjwa wa kisukari na watanzania wote kuweza kutumia sukari hiyo yenye radha sawa na sukari ya kawaida bila kupata matatizo ya kiafya.

Akizungumza katika uzinduzi wa bidhaa hizo uliofanyika Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Abacus Pharma (A) LTD, Ramesh Babu alisema bidhaa hizo zimesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza matumizi makubwa ya sukari katika vyakula. 
 
Alisema bidhaa hizo zimetengenezwa mahususi ili kukabiliana na ongezeko la sukari mwilini na hivi sasa zinapatikana kwa bei ya chini katika soko la nchi za Tanzania, Uganda, Kenya, Rwanda na Burundi na kuwa bei hizo zipo kuanzia shilingi,4200, 4,500, 5,700, 8,850 na za bei ya juu ni shilingi 13,000 na kuwa zinategemea bidhaa husika.
 
“Bidhaa hizi zipo za aina mbili za sugar free gold  ambazo hutumika katika chai, uji, na vinywaji baridi tu  na sugar free natura hutumika katika baking, kupikia vyakula vinavyohitaji sukari katika upishi na pia hutumika katika chai, uji na vinywaji baridi na matumizi yake ni rahisi sana,” amesema  Babu.
 
Amesema kwa Tanzania bidhaa hizo zimeanza kuchukua soko kubwa baada ya wananchi kuona umuhimu wake na hivyo wanategemea muitikio utaendelea kuwa mkubwa.
 

Ameongeza kuwa, lengo kubwa la kampuni hiyo kusambaza bidhaa hizo ni kusaidia jamii kuelewa matumizi ya bidhaa hizo ambazo hazina sukari ingawa zina ladha ya sukari kama ile ya kawaida  na kwamba bidhaa hizo zimethibitishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Akizungumzia bidhaa hiyo ya ‘Sugar Free’ Meneja wa Masoko Kampuni ya ABACUS Pharm Jeremiah Bwana, amesema kuwa free sugar ni sukari isiyokuwa na Calories (Calories 0%) jambo ambalo linawapa nafasi watanzania kunufaika na sugar free.

Amesema kuwa uwepo wa free sugar itawapa furaha watu wenye matatizo ya kisukari ambao muda mrefu wamekuwa hawatumii sukari ya kawaida kutokana na matatizo ya kiafya.

“italeta ahuweni kwa wagonjwa wa kisukari ambao awali walikuwa hawatumii sukari, lakini sasa itakuwa rafiki kutokana free sugar ina radha sawa na bidhaa nyengine” amesema Jeremiah.

Hata hivyo imeeleza kuwa uwepo wa ‘sugar free’ ni muhimu sana kutokana ugonjwa kisukari hapa nchini ni mkubwa sana, kwani   Tanzania inashika nafasi ya tano duniani katika nchi ambazo wananchi wake wanaumwa ugonjwa wa kisukari.

Kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi pamoja na kula vyakula ambavyo sio rafiki kwa binadamu imeelezwa ni miongoni mwa sababu zinazosababisha kuongezeka kwa ugonjwa kisukari.

Familia nyingi zimekuwa zikitumia asilimia 25 katika pato lake kwa ajili ya kumuhudumia mgonjwa wa kisukari kitu ambacho gharama hiyo ni kubwa sana.

Akizungumza katika uzinduzi wa bidhaa ya Sugar Free, Mkuu wa Kitendo Cha Kisukari kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dk Mohamed Juma, amesema kuwepo kwa bidhaa ya free sugar itaweza kusaidia katika kutatua changamoto kadha zilizokuwepo hapa nchini.

Amesema kuwa bidhaa hiyo ni nzuri kwani radha yake nipo sawa na sukari ya kawaida katika mtumizi yoyote ambayo mtumiaji amekusudia kutumia.

“kutokana na umuhimu wa uwepo wa bidhaa ya Sugar Free itasaidia kutatua changamoto ambazo zipi katika kufanikisha kuondoa matatizo ambayo yamekuwa kwa muda mrefu” amesema Dk Mohamed.

Hata hivyo Mratibu wa kisukari Wilaya ya Ilala, Daktari Bigwa Dk Bushara Faraja, amesema sugar free ni msaada mkubwa kwa wagonjwa ambao wanaumwa ugonjwa kisukari.

Amesema kuwa baada ya kuja bidhaa ya Sugar Free kutoka Kampuni ya ABACU wataendelea kutumia sukari bila kupata madhara yoyote ya kiafya na kutofauti na awali.

“Bidhaa ya Sugar free ni nzuri kwani inampa mtu yoyote fursa ya kuweza kutumia bila kuingiza kitu chochote mwilini mbacho sio rafiki” amesema Dk Faraja.

                     
 Daktari Bingwa wa Magonjwa ya homoni na Kisukari kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Faraja Chiwanga akikabidhiwa zawadi.
 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Abacus Pharma (A) LTD, Ramesh Babu, akipatiwa zawadi.

 Wafanyakazi wa kampuni hiyo wakiwa kwenye uzinduzi huo.
 Uzinduzi ukiendelea.
  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Abacus Pharma (A) LTD, Ramesh Babu, akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
 Wadau wakiwa kwenye uzinduzi huo.
 Ni furaha tupu katika uzinduzi huo.
 Uzinduzi huo.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here