WINGU LA HABARI.
Shirikisho la soka Duniani (FIFA ) limetoa viwango vipya vya soka duniani ambapo Tanzania imeshuka kwa nafasi tano kutoka nafasi ya 120 hadi 125.
Kikosi cha timu ya Soka ya Ujerumani
Katika orodha hiyo sasa Ujerumani wamerudi tena kuchukua nafasi yao ya kwanza ambayo hapo mwanzo ilienda kwa timu ya Brazil.
Brazil waliokuwa wakishika nafasi ya kwanza sasa wamekuwa nafasi ya pili huku Ureno waliokuwa nafasi ya sita sasa wako nafasi ya 3 na Argentina waliokuwa nafasi ya 3 wameshuka hadi 4. Waliokuwa nafasi ya 3 wameshuka hadi 4.
Ubelgiji wamepanda hadi nafasi ya 5 kutoka 9 walipokuwa huku nafasi ya 6 ikienda kwa Poland, timu ya taifa ya Swiztrland wako katika nafasi ya 7 huku ya 8 ikikamatwa na Ufaransa.
Mabingwa wa Amerika Kusini timu ya taifa ya Chile wako nafasi ya 9 huku wanaofunga orodha ya 10 bora ni timu ya taifa kutoka bara la America timu ya Colombia.
Timu ya taifa ya Uingereza ambayo imeshuka hadi nafasi ya 15 ikiwa ni baada ya miaka 17 kufika katika hatua hiyo na wakipitwa na Wales walioko 13.
Kwa upande wa kumi bora ya Africa, Misri wanaongoza wakifuatiwa na Tunisia huku Wasenegal wakiwa katika nafasi ya 3, ya 4 ikienda kwa DRC.
Nigeria wako nafasi ya 5, wakifuatiwa na mabingwa wa Africa timu ya taifa ya Cameroon huku Burkina Fasso wakishika namba 7, 8 ni Ghana, 9 Ivory Coast na 10 ni Morocco.
No comments:
Post a Comment