MKUU WA MKOA MBEYA MHE. MAKALLA ATOA MAAGIZO KWA WATAALAM WA KILIMO. - WINGU LA HABARI- ONLINE

Breaking

TANGAZO

TANGAZO
Sugar free

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Thursday, December 21, 2017

MKUU WA MKOA MBEYA MHE. MAKALLA ATOA MAAGIZO KWA WATAALAM WA KILIMO.

WINGU LA HABARI, MBEYA 
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla amepiga marufuku wataalam wa kilimo kukaa ofisini na kwamba ni kinyume cha sheria.

Pia amewaagiza wakurugenzi, wakuu wa wilaya zote mkoani hapa  kuhakikisha wanatenga hekta 100 kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda ikiwa ni utekelezaji  sera ya uchumi wa  viwanda.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla katika akimsikiliza mkazi wa Kijiji cha Kikondo, Joba  Chriss  baada ya kukagua barabara yenye urefu wa kilometa zaidi ya 200   na maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya Sekta ya uwekezaji.

"Wataalam  wa kilimo ni marufuku kukaa ofisini, sasa ni kuelekeza nguvu kwa wakulima. Kitendo cha kutotekeleza majukumu yao ni kinyume cha sheria,"amesema.

Ametoa agizo hilo leo jijini Mbeya alipokuwa katika mahojiano maalum na matukio360 na kwamba ni lazima maeneo yatengwe ili kuhakikisha  serikali inafikia malengo ya kutekeleza uchumi wa viwanda hususan kuwandaa wakulima kuzalisha mazoa yaliyo na tija

"Sera ya viwanda itafikiwa endapo wakulima watakuwa na afya njema na Serikali sasa inawekeza zaidi katika sekta ya kilimo  hivyo ni jukumu lenu wakurugenzi, wakuu wa wilaya kusimamia na kutenga maeneo kwa ajili ya uwekezaji,"amesema Makalla.

Pia amewaagiza  kuweka kipaumbele  upatikanaji wa pembejeo kwa wakati, wakulima kupewa elimu ya kilimo kutoka kwa wataalam na si kuwaacha tu.

Makalla, pia amewataka  watendaji kuacha mara moja  tabia ya

kuwakaimisha maofisa ugani nafasi zao  jambo linalosababisha kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavvyo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here