WINGU LA HABARI
Na
Noel Rukanuga
Kampuni
ya SBC Tanzania Limited imewapa fursa watanzania ya Mamilioni baada ya
kuanzisha shindano la ‘Jishindie Mamilion’ linalohusu soda aina ya Pepsi, Mirinda
Orange, Mirinda Fruity,Mirinda Green Apple, Mountain Dew(300ml) pamoja na
Seven up ambazo zinaujazo ujazo wa mililita 350.
Shindano hilo ambalo litaanza Desemba 4 mwaka huu mpaka Desemba 1, 2018 katika baadhi ya Mikoa
nchini ikiwemo Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Dodoma,Tanga, Lindi pamoja na
Mtwara.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Meneja Mfunzo na Uwezeshaji wa Kampuni ya SBC Tanzania
Limited Rashid Chenja, amesema kuwa
vizibo vya shindano hilo vitakuwa na rangi ya silva ambapo kutakuwa na zawadi za pesa taslimu kuanzia shilingi
1,000,000/,500,000/-,10,000/-,5000/-,1000/- pamoja na soda ya bure.
“lengo
la shindano haya ni kuongeza unywaji wa soda na kuipatia jamii sehemu ya faida
ili kuwawezesha kujikomboa kiuchumi” amesema Chenja.
Meneja Mfunzo na Uwezeshaji wa Kampuni ya SBC Tanzania
Limited Rashid Chenja upande wa kulia
akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Amefafanua
kuwa ili mteja ajishindie zawadi anapaswa kununua soda za kampuni hiyo kisha abandue
ganda ndani ya kizibo akikuta maandishi aidha ya shilingi 1,000,000/-, 500, 000/-10,000/-1000/-shilingi
5000/-1000/-, na soda ya bure na atapatiwa kwa aliyeuza soda.
Kampuni
ya SBC Tanzania Limited ni kampuni inayotengeneza kusambazaji vinywaji mbalimbali
hapa nchini ikiwemo soda ya Pepsi, Mirinda,7up na Mountain Dew na vinywaji
vingine
No comments:
Post a Comment