Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii, Ephraim Kwesigabo kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS)
WINGU LA HABARI
Na Noel Rukanuga.
Mfumo wa bei wa taifa kwa mwezi Novemba mwaka huu umepungua kutoka
asilimia 5.1 katika mwezi Oktoba hadi kufika asilimia 4.4.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii,
Ephraim Kwesigabo kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) amesema kuwa hali hiyo inamaanisha kuwa kasi
ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi novemba
mwaka huu imepungua ikilinganisha na kasi ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi oktoba mwaka huu.
“Kupungua huko imetokana na mfumuko wa bei wa taifa unapima kiwango cha
kasi ya mabadiliko ya bei ya bidhaa pamoja na huduma zote zinazotumiwa na kaya
binafsi hapa nchini’’ Kwesigabo
Ameeleza kuwa kupungua kwa mfumuko wa bei
kumechangiwa na kupungua kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula kwa kipindi
kilichoishia mwezi novemba mwaka huu zikilinganishwa na bei za mwezi novemba
mwaka wa jana.
Amefafanua kuwa baadhi za vyakula zilizochangia
kupungua kwa mfumuko wa bei ni pamoja na nyama ya ngombe kwa asilimia 5.4,
samaki wabichi asilimia 22.2, mbogamboga kwa asilimia 3.9, viazi mviringo kwa
asilimia 14, mihogo mibichi kwa asilimia 24.8 pamoja na viazi vitamu kwa
asilimia 13.4.
Hata hivyo mfumuko wa bei nchini Tanzania una
mwelekeo unaofafana na baadhi ya nchi nyengine za Afrika Mashariki ambapo
katika nchi ya Kenya mfumuko wa bei kwa mwezi novemba mwaka huu umepungua hadi
kufikia asilimia 4.73 kutoka asilimia 5.72.
Nchini Uganda mfumuko wa bei umepungua na kufikia
asilimia 4 mwezi novemba mwaka huu kutoka asilimia 4.8 kwa mwezi Oktoba mwaka
huu.
No comments:
Post a Comment