MAAMBUKIZI YA VVU WAPUNGUA ASILIMIA NNE. - WINGU LA HABARI- ONLINE

Breaking

TANGAZO

TANGAZO
Sugar free

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Friday, December 1, 2017

MAAMBUKIZI YA VVU WAPUNGUA ASILIMIA NNE.



Maambukizi  ya ugonjwa wa UKIMWI nchini umepungua kutoka utoka asilimia 5.1 mwaka 2011/2012 hadi kufikia asilimia 4.7 mwaka 2016/2017.

Haya yamebainishwa leo katika siku ya ugonjwa wa ukimwi dunia ambapo maadhimisho hayo yalifanyika katika viwanjwa vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa kuzindua matokeo ya Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania kwa Mwaka 2016/2017, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa kwa mujibu wa utafiti huo inakadiriwa kuwa watanzania wapatao million 1.4 wanaishi na virusi vya ukimwi.

Amesema kuwa  utafiti huo unaonesha kuwa kiwango cha maambukizi kwa wanawake ni asilimia 6.5 huku wanaume ukiwa asilimia 3.5.

Mhe. Samia Suluhu amesisitiza kuwa kupungua kwa kiwango cha maambukizi hakumaniishi kuwa UKIMWI umeisha bali ni matokeo ya jitihada zilizofanywa na Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine ikiwemo wananchi katika kujilinda dhidi ya maambukizi mapya.

Awali akitoa maelezo kuhusu utafiti huo, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa, amesema kuwa huo ni utafiti wa nne kufanyika hapa nchini, ambapo kwa mara ya kwanza ulifanyika mwaka 2003/04 ambao ulionesha kiwango cha maambukizi kilikuwa asilimia 7 na kufuatiwa na tafiti nyingine za miaka ya 2007/08 na 2011/12 iliyoonesha maabukizi ya asilimia 5.1

Ameeleza kuwa utafiti huu ulihusisha kaya 16,198 na kujumuisha wanakaya wote waliokuwa kwenye kaya wakilishi zilizochaguliwa na umegharimu kiasi cha Shillingi 7.4 bilioni ambazo zimetolewa na Serikali ya Marekani chini ya Mfuko wa Raiswa Dharura wa Kupambana na UKIMWI (President’s Emergency Plan for AIDS Relief – PEPFAR).

Naye Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Mhe. Jenista Mhagama  amemuagiza mkurugenzi wa TACAID  hadi kuffikia mwaka 2018 aweze kuanzisha kampeni itakayo wafanya wanaume  kujitokeza kwa wingi katika upimaji wa ugonjwa wa UKIMWI.

Utafiti huo umebainisha mikoa ambayo kiwango cha maambukizi ya VVU ni zaidi ya asilimia 10 ni Iringa yenye maambukizi ya asilimia 11.3 na Njombe yenye asilimia 11.4 huku mikoa yote ya Tanzania Zanzibar ikiwa na maambukizi ya ukimwi ni chini ya asilimia 1.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here