Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Robert Boaz akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam
WINGU LA HABARI
Kuelekea kipindi cha sikukuu za Krismasi na mwakampya Jeshi la Polisi limesema , limepanga mikakati madhubiti ya kukabiliana na matishio ya amani na utulivu pamoja na kudhibiti vyanzo vyote vya ajali za barabarani , likitoa takwimu za matukio ya uharifu kwa mwaka 2016 na 2017 kuwa yamepungua kwa asilimia 9. 4.
Hayo yame bainishwa leo na mkurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya jinai DCI Robert Boazi,wakati akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya Polis jijini Dar es salaam nakusema kuwa pamoja na kupungua kwa asilimia 9 makosa ya Mauaji, ulawiti, wizi wa watoto, kutua watoto Kunajisi, ubakaji na usafirishaji binadamu yameongezeka .
'' Makosa hayo kwa mwaka 2016 yalikuwa 11, 794 na mwaka huu kwa kipindi kama hicho yameripotiwa makosa 11, 620 sawa na ongezeko la makosa 107 ambayo ni sawa na 0.9%.''alisema Boazi.
Kwa upande wa ajali za barabarani Boazi amesema makosa 9,550 mwaka 2016 yaliripotiwa na 2017 matukio yaliyoripotiwa ni 5,537 ambayo ni sawa na pungufu ya matukio 4013 sawa na asilimia 42 , na kueleza kuwa chanzo chake ni makosa ya kibinadamu, sababu za kimazingira na ubovu wa vyombo vya usafiri.
Pamoja na hayo DCI Boazi akijibu maswal ya waandishi kuhusu kupotea kwa Ben saanane ,mwandishi wa mwananchi Azory Gwanda ,kupigwa Risasi Tundu Lisu pamoja tuhuma za uchochezi zinazo mkabili Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CHADEMA ambaye pia ni Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Edward Lowasa amesema, Jeshi hilo linaendelea na uchunguzi wa matukio hayo na kuwa taka wanachi kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo ili kufanisha kupatikana kwa waharifu, na kwamba upelelezi wa tuhuma za Lowasa unaendelea na ukikamilika at a fikishwa mahakamani.
No comments:
Post a Comment