Balozi wa Jerumani Amb.Detlef Waechte akutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh. Paul Makonda kuhusu changamoto zinazokabili mkoa huu.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo Mh Makonda amesema Balozi huyo amtembelea Tanzania na kumtaka aeleze changamoto zinazowakabili, na kuhaidi kuzitekeleza kadri awezavyo.
Aidha amesema amemueleza balozi huyo changamoto katika sekta ya Afya,katika sekta ya elimu ambapo kuna ujenzi wa ofisi za walimu, pamoja na kupambana na madawa ya kulevya, ambapo ameahidi kushirikiana kikamilifu katika kupunguza na kuondo kabisa tatizo hilo.
Pia amemshukuru sambamba na kufurahishwa na balozi huyo kuja kwake,na kuweza kumtembelea, na kuweza kuangalia changamoto zinazooabili mkoa huu kikamilifu.
Katika tukio jingine Mh. Paul Makonda amekutana na Mkuu wa Meli ya madktari wanaotoa huduma ya Upimaji na Matibabu bure katika bandari ya Dar es Salaam, ambapo wameangalia changamoto inayowakabali ambayo ni watu kujitokeza kwa wingi kuliko idadi iliyokusudiwa kuhudumia watu mia sita tu.(600) ndani ya siku zote tano.
Amesema kutokana na changamoto hiyo wameongeza nguvu kazi ambapo huduma ya Upimaji itatolewa katika kituo cha polisi central, na maeneo mawili ambapo yatarahisisha huduma na kufanikisha wananchi wote waliofika na kupatiwa namba wanaweza kupatiwa huduma kikamilifu.
"Niwashukuru wananchi kujitokeza kwa wingi katika kupewa huduma hii,kutokana na watu wengi kuitikia wito hatuwezi kuwarudisha nyumbani tunahangaika ili waweze kupata huduma kutokana na mwananchi amekuja na anauhitaji ivyo hawezi rudi na ugonjwa wake hivyo tumeandaa vituo vitatu kutokana kwenye laini moja ili kuweza kuwahudimia wananchi wengi zaidi" Amesema Makonda
Aidha amesema lengo ni kuwa kila mwananchi aweze kuapiwa huduma na kuwa na afya njema, hivyo amewataka wanaopatiwa matibabu waweze kufuata maelekezo ya madaktari ili waweze kurudi katika hali ya kawaida.
Kwa upande wake Balozi wa ujerumani nchini Tanzania Amb.Detlef Waechte ameahidi kuyafanyia kazi yale waliyoyajadili na mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ikiwemo kuunga mkono jutihada za mkuu wa mkoa katika kujenga Ofisi za walimu wa Dar es salaam
No comments:
Post a Comment