Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ampa mwezi mmoja afisa Aridhi wa Wawilaya ya Namtumbo Bwana Maurus Year kuhakikisha ametatua tatizo la Ardhi lilio dumu miaka kumi katika Wilaya ya Namtumbo.Waziri Mkuu ametoa agizo hilo jana Novemba 23/2017 katika mkutano wa hadhara Wilayani Namtumbo Mkoa wa Ruvuma.
Waziri Mkuu. Kassim Majaliwa akiongea na Wananchi wa kijiji cha Chomolo Wilaya ya Namtumbo wakati walipo simamisha msafara wake leo Novemba 24/2017 wakati alipo kuwa akielekea katika ziara ya kikazi katika wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma.
PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU
………………
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameweka jiwe la msingi katika ujenzi wa miradi miwili ya maji katika vijiji viwili vya Rahaleo na Mbungulaji kwenye kata ya Kalulu yenye thamani ya sh. Milioni 112 na kuahidi kumaliza kero ya maji wilayani Tunduru.
Amesema Serikali imedhamiria kumaliza tatizo la upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, hivyo amewaomba wananchi kuendelea kuwa na imani na Serikali yao.
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Ijumaa, Novemba 24, 2017) mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa miradi ya maji katika vijiji hivyo kwa lengo la kumaliza changamoto ya umatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika maeneo hayo.
Amesema ujenzi wa miradi hiyo ni utekelezaji wa Kampeni ya Rais Dkt. John Magufuli ya kumtua mama ndoo kichwani yenye lengo la kuwafikishia wananchi huduma ya maji safi na salama katika umbali usiozidi mita 400 kutoka kwenye makazi yao.
“Nataka maji haya yaende kwa wananchi si wananchi wayafuate, hivyo mara baada ya kukamilika ujenzi wa mradi huu Halmashauri ijenge mtandao wa mabomba yatakayosafirisha maji kutoka eneo la mradi hadi kwenye vioksi na kuyafikisha katika makazi ya wananchi.”
Pia ametoa wito kwa wazee wa vijiji hivyo kwa kushirikiana na vijana kuhakikisha wanalinda mradi huo kwa kutokata miti kwenye maeneo yote yanayozunguka vyanzo vya maji ili kuepusha ukame. Ameagiza ipandwe miti kwenye maeneo hayo ili kuhifadhi mazingira.
Wakati huo huo, Waziri Mkuu amewataka watumishi wa umma kuhakikisha wanatekeleza ipasavyo majukumu yao ikiwa ni pamoja na kufanya kazi ya kuwatumikia wasnanchi bila ya ubaguzi wa dini, rangi na itikadi za vyama.
Amesema Serikali haitaki kusikia mwananchi anakwenda kufuata huduma katika ofisi zao na kuzungushwa kwa muda mrefu bila ya kuhudumiwa. “Serikali hii haitaki wananchi wake hususan wanyonge wasumbuliwe tukikubaini tunakuondoa.”
Waziri Mkuu ameongeza kwamba “Serikali hii haidekezi wala kuwaonea aibu watumishi wasiowajibika katika kuwatumikia wananchi. Serikali hii haitamuhifadhi mtu atakayeshindwa kufanya kazi, tunataka kazi tu na asiyefanya kazi na asile ndiyo maana tunawaondo watumishi wazembe wote.”
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
IJUMAA, NOVEMBA 24, 2017.
No comments:
Post a Comment