Dar es Salaam, Novemba 24, 2017:
Serikali inautaarifu umma kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ataungana na viongozi wa mataifa mbalimbali kuhudhuria sherehe za kuapishwa Mhe. Uhuru Kenyatta kuwa Rais wa Jamhuri ya Kenya kwa kipindi cha awamu ya pili.
Mhe. Kenyatta ataapishwa siku ya Jumanne, Novemba 28, 2017, jijini Nairobi, baada ya ushindi alioupata katika uchaguzi wa marudio uliofanyika Oktoba 26 mwaka huu nchini humo.
Imetolewa na:
Dkt. Hassan Abbasi
Mkurugenzi, Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali.
No comments:
Post a Comment