Na mwandishi wetu
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemhukumu meneja wa Nyanza Commercial Farm, Dilipkumar Pater kulipa faini ya Sh 534 milioni ama kutumikia kifungo cha miaka 20 jela baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kupatikana na kucha 17 za Simba.
Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Cyprian Mkeha, baada ya kusikiliza ushahidi uliotolewa na mashahidi wanne wa pande wa mashtaka, vielelezo vitatu na utetezi wa mshtakiwa mwenyewe Pater ambaye ni raia wa India.
Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mkeha alisema mahakama imemkuta mshtakiwa huyo na hatia baada ya upande wa mashtaka kuthibitisha kesi yao pasipo kuacha shaka na kuhukumiwa.
Vielelezo hivyo vitatu ni kucha za simba, hati ya ukamataji na cheti cha kutathmini kucha hizo.
Hatua hivyo mshtakiwa huyo walishindwa kulipa faini na kupelekwa gerezani.
Kabla ya hukumu hiyo kutolewa mshtakiwa huyo alijitetea kuwa yeye ni mgonjwa na anategemewa na familia.
Kwa mujibu wa kesi hiyo , mshtakiwa huyo anadaiwa kuwa alitenda kosa hilo Novemba 19, mwaka 2016, katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Pater anadaiwa kuwa siku hiyo alikutwa na kucha 17 za Simba zenye thamani ya Sh 53,483,500 bila ya kuwa na kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyamapori.
No comments:
Post a Comment