![]() |
| Mchezaji wa tenis Roger Federe mwenye furaha . |
Nyota wa tenisi Roger Federer anatarajia kushirikiana
na bingwa wa zamani wa Wimbledon Martina Hingis kutoka Uswizi katika mashindano
ya jinsia mchanganyiko wa Michezo ya Olimpiki ya Rio 2016.
Federer,
34, na Hingis walicheza mara ya mwisho pamoja katika Kombe la Hopman nchini
Australia 2001.
Bingwa
huyo mara 17 wa Grand Slam amesema ana
kuwa anafuraha furaha sana”.
"Nilimuenzi
sana nilipokuwa mchanga. Niliamini alikuwa na kipaji adimu,” aliongeza Federer,
ambaye ni mdogo wa Hingis kwa mwaka mmoja.
“Tuko
karibu sawa kwa umri na alikuwa akishinda mataji ya Grand Slam nilipokuwa bado
kituo cha taifa cha tenisi. Nilishangazwa sana na ustadi wake.”
Image copyrightAPImage captionHingis alitwaa taji la
Wimbledon mwaka 1997 akiwa na umri wa miaka 16
Hingis,
35, alishinda mataji matano ya Grand Slam katika uchezaji wake, moja akilitwaa
Wimbledon mwaka 1997 akiwa na umri wa miaka 16.
Alikuwa
amestaafu mara mbili awali lakini akarejea mchezoni tena 2013 na amekuwa
akifanikiwa mashindanoni.

No comments:
Post a Comment