Rooney alikuwa ametishia kuhama United lakini mwishowe akatia
saini mkataba wa kulipwa ujira wa £250,000 kila wiki.
"Niliwaambia sikudhani ilikuwa haki kwa Rooney kulipwa
mshahara mara mbili ya mshahara wangu,” Ferguson amesema kwenye kitabu kipya.
Aidha mwenyekiti
mwenza wa Man United Joel Glazer alisema kuwa walikubaliana Roney lakini hakuwa zamila yao kufanya hivyo.
'haikuwa rahisi, tuliamua kuendelea naye kwa sababua hakuna mchezaji anayefaa kulipwa mshahara
mkubwa kunishinda.”
Kwenye kitabu chake kipya kuhusu usimamizi chenye jina la Leading ,
Ferguson anasimulia kuhusu kipindi cha mpito alipoondoka Manchester United 2013
baada ya kuwa kwenye usukani miaka 26, akisema: "Tungeliisimamia vyema.”
Raia huyo wa Scotland, aliyeshinda mataji mawili ya Ligi ya
Kilabu Bingwa Ulaya, mataji 13 ya Ligi ya Premier, vikombe vitano vya FA na
vikombe vinne vya League, alirithiwa David Moyes, aliyefutwa miezi 10 baadaye.
Lakini mkufunzi huyo mwenye umri wa miaka 73 anasema alitaka pia
kuzungumza na aliyekuwa kocha wa Barcelona ambaye sasa ananoa Bayern Munich Pep
Guardiola kabla yake kumteua Moyes.

No comments:
Post a Comment