MGOMBEA urais wa Zanzibar
kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Ali Mohamed Shein amesema
atahakikisha Zanzibar inajitosheleza kwa chakula na kupunguza uagizaji wa
chakula nje ya nchi, kwa kuimarisha kilimo cha umwagiliaji mpunga mashambani.
Dk
Shein alisema hayo Tunguu katika Wilaya ya Kati Unguja wakati akihutubia
mkutano wa hadhara wa kampeni na kusema wakati umefika kwa Zanzibar
kujitosheleza kwa chakula na kupunguza uagiziaji chakula nje ya nchi ambao
unaligharimu taifa fedha nyingi za kigeni.
Alizitaja
juhudi zilizochukuliwa hadi sasa ni kuanzishwa kwa mashamba darasa 1,200 ya
mpunga ambapo tani 674,334 za mazao ya chakula zimezalishwa ukilinganisha na
tani 346,535 katika mwaka 2014, ongezeko hilo limefikia asilimia 95.
Alifafanua
kuwa jumla ya matrekta 45 yamenunuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar(SMZ) huku matrekta makongwe 37 yakifanyiwa matengenezo makubwa pamoja
na mashine za kuvuna mpunga 14 zikinunuliwa.
Aidha,
alisema eneo la uzalishaji mpunga limeongezeka kutoka hekta 10,000 mwaka 2010
na kufikia hekta 34,000 mwaka huu huku akisisitiza kwamba kiwango cha
uzalishaji wa mpunga kimeongezeka kutoka tani 20,000 hadi tani 33,655 pamoja na
kuongezeka kwa idadi ya kaya zinazozalisha kilimo hicho na kufikia 10,000 mwaka
2010 hadi kufikia 70,000 mwaka 2014.
“Hizo
ndizo juhudi zetu na mipango yetu katika kuimarisha kilimo cha umwagiliaji
mashambani cha mpunga na kuona kwamba tunapunguza uagiziaji nje ya nchi kwa
kuwawezesha wakulima wetu,” alisema Dk Shein anayeomba muhula wa pili na mwisho
wa urais Zanzibar.
Alisema
malengo yamewekwa hadi kufikia 2017- 2018, asilimia 60 ya mahitaji ya kilimo
cha mpunga kiwe kinazalishwa nchini ambapo mabonde ya mpunga yaliyopo Cheju,
Mtemela Pemba yataimarishwa.
Alieleza
kuwa matumaini yapo makubwa zaidi baada ya serikali kuchukua juhudi za
kuimarisha Kituo cha Kilimo cha Kizimbani kwa kupokea idadi kubwa ya wanafunzi
wa cheti kutoka 300 katika mwaka 2010 hadi kufikia 741 katika mwaka 2014 huku
mafunzo ya Stashahada katika fani ya uzalishaji mifugo na uzalishaji wa mazao
ya kilimo mjumuishi yameanza kufundishwa kwa wanafunz.

No comments:
Post a Comment