Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii, Ephraim Kwesigabo akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
WINGU
LA HABARI
NA NOEL
RUKANUGA, DAR ES SALAAM.
Mfumuko
wa bei wa Taifa kwa mwezi februari mwaka huu umeongezeka hadi kufikia asilimia
4.1 ukilinganisha na asilimia 4 katika mwezi januari.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Sensa ya Watu
na Takwimu za Jamii, Ephraim Kwesigabo,
amesema kuwa kuongezeka kwa mfumuko wa bei kwa mwezi februari mwaka huu kumechangiwa
na kuongezeka kwa mfumuko wa bei kwa bidhaa zisizo za vyakula.
Amesema
kuwa bidhaa hizo zisizo za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa mfumuko wa bei
ni pamoja na mkaa asilimia 17.6, gesi ya kupikia kwa asilimia 11.1, mafuta ya
taa asilimia 9.9, petroli asilimia 13.1.
Bidhaa
nyengine ni dizeli kwa asilimia 11.3, huduma za meno kwa asilimia 12.9, viatu
asilimia 3.4, mavazi ya wanaume asilimia 3.4 huku mavazi ya wanawake yakiwa asilimia
3.8.
“Kuongezeka
kwa mfumuko wa bei kwa mwezi februari mwaka huu kumechangiwa na bidhaa zisizo
za vyakula ingawa kuna bidhaa chache za vyakula zilizochangia” amesema
Kwesigabo.
Katika
hatua nyengine amefafanua kuwa hali ya mfumuko wa bei kwa baadhi ya Nchi za
Afrika Mashariki kwa mwezi februari mwaka huu umepungua hadi kufikia asilimia 2.1
kutoka asilimia 3 kwa nchi ya Uganda.
Kwa
upande wa Kenya mfumuko wa bei umepungua hadi kufikia asilimia 4.46 kutoka
asilimia asilimia 4.83.
No comments:
Post a Comment