Mkuu
wa Kitengo cha Ukuaji Shirikishi na Masuala ya Ustawi wa Jamii wa Mpango
wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP), Ernest
Salla akizungmza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Mratibu
wa United National Global Compact Networt Tanzania (UNGCNT) Emmanuel Nnko akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Huduma kwa Wanachama Tanzania (TPSF) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
WINGU
LA HABARI.
NA NOEL
RUKANUGA, DAR ES SALAAM.
Mpango
wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP) imezitaka Taasisi na sekta binafsi kufanya
kazi kwa ushirikiano ili kusaidia kufanikisha maendeleo endelevu katika nyanja mbalimbali
ikiwemo uchumi.
Akizungumza
na watendaji wakuu wa taasisi na sekta binafsi Mkuu wa Kitengo cha Ukuaji
Shirikishi na Masuala ya Ustawi wa Jamii (UNDP), Ernest Salla amesema kuwa leo
wameamua kukutana na watendaji hao ili kuwapa elimu ya kufanikisha maendeleo
endelevu hapa nchini.
Amesema
kuwa katika kufanikisha mpango huo, kila mmoja anatakiwa kushiriki kikamilifu
ili kufanikisha maendeleo endelevu na kupiga hatua katika sekta zote ikiwemo
uchumi.
“Kila
mtu anatakiwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo ili kuwe na uchumi, kipato,
kuondoa umaskini, matabaka, na katika utekelezaji wa kufikia maendeleo endelevu
kuna kazi kubwa ambayo inapaswa kufanyika kwa ushirikiano” amesema Salla.
Kwa
upande wake Mratibu wa United National Global Compact Networt Tanzania (UNGCNT)
Emmanuel Nnko, amesema kuwa lengo kubwa la kukutana na watendaji wa sekta
binafsi ni kuwashirikisha katika kusaidia maendeleo endelevu ya taifa.
Amesema
kuwa kukutana na watendaji hao wanapata fursa ya kuwaelimisha na kuwaelekeza
vitu ambavyo wanapaswa kufanya ili kufanikisha maendeleo endelevu.
Nnko
amefafanua kuwa kuna fursa nyingi ambazo zinapaswa kufanya na makapuni pamoja
na taasisi binafsi, hivyo elimu hiyo itawasaidia katika kufanisha fursa hizo.
Ameeleza
kuwa kitu cha muhimu kinachopaswa kufanywa na watendaji wa sekta binafsi ni kufata
kanuni pamoja na kuchukua hatua juu yale watakayozungumzia katika kupeana elimu
ambayo ni rafiki kwa maendeleo ya taifa.
“Ili
tuweze kwenda na kufanikiwa katika maendeleo endelevu lazima wadau wote ikiwemo
serikali, sekta binafsi, taasisi zisizo za kiserikali pamoja na wananchi kushirikiana
pamoja ili kupata afya bora, usawa wa kijinsia pamoja na kutuza mazingira yetu”
amesema Nnko.
Amebainisha
kuwa lengo kubwa ambalo limebeba malengo yote ni katika kanuni ni lengo la 17
ambalo ni ushirikiano na imeonekana ni nguzo muhimu.
Mkurugenzi wa Huduma kwa Wanachama Tanzania (TPSF) Lanis Accan ambaye anatoka sekta binafsi, amesema kuwa ushirikiano ni jambo la muhimu kutokana ni nguzo ya kufika mafanikio.
No comments:
Post a Comment