Waziri wa Elimu,Sayansi,na Teknolojia Tanzania Prof.Joyce Lazaro Ndalichako akiwa kwenye picha ya pamoja.
WINGU LA HABARI
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Serikali ya China imefanikiwa kutumia bilioni 90 katika kufanikisha ujenzi wa maktaba mpya ya kisasa iliyojegwa katika Chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kwa ajili ya kusaidia kuboresha elimu hapa nchini.
Hayo yameelezwa leo na Waziri wa Elimu, Sayansi,na Teknolojia Tanzania Prof. Joyce Lazaro Ndalichako wakati akifanya ziara ya kutembelea wafanyakazi wa ujenzi wa maktaba hiyo, ambapo amesema itawasaidia wanafunzi kusoma na kupata mafunzo na ujuzi mbalimbali.
Pro. Ndalichako amesema maktaba hiyo ni ya kisasa kwani itaweza kuhifadhi vitabu zaidi ya laki nane pamoja kuweka vifaa maalum vya kujifunzia kwa watu wenye mahitaji maalum.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Pro William Anangisye, amesema wanaishukuru serikali kuwa na mipango yake mizuri inayolenga kuboresha elimu nchini.
Wang Ke ni Balozi wa China nchini Tanzania amesema Tanzania kama nchi inayoendelea wamependa kuisaidia katika kujenga maktaba hiyo na hivyo itasaidia kuwajengea uwezeo wanafunzi ambao wanakwenda kujisomea kwenye maktaba hiyo.
Ujenzi wa maktaba hiyo unatajiwa kumalizika mwezi Juai mwaka huu ambapo itakuwa na uwezo mkubwa Africa Mashariki na barani Afrika kwa ujumla.
Katika hatu nyingine Pro.Ndalichako amesema wanategemea hivi karibu kuanza mradi wa ujenzi wa chuo Kikubwa cha kisasa cha mafunzo ya Ufundi Stadi cha veta mkoani Kagera ambapo wamekwisha saini makubaliano na Serikali ya China watawapatia fedha za kitanzania shilingi bill 22 ili kufanikisha mradi huo
No comments:
Post a Comment