WINGU LA HABARI
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM.
Baada ya kupoteza mchezo wa nusu fainali kombe la Mapinduzi dhidi ya URA ya Uganda kwa michwaju ya penati, klabu ya Yanga imewasili jijini Dar es Salaam wakitokea viziwani Zanzibar huku mashabiki wa soka wakipeleka lawama zao kwa mshambuliaji wa Kimataifa Mzambia, Obrey Chirwa.
Sauti za mashabiki wa soka walisikika wakisema ahsante Chirwa, huku wengine wakibeba mabango yenye ujumbe wa ‘AHSANTE CHIRWA) jambo ambalo lilipelekea mchezaji huyo wa kimataifa raia zambia kupewa ulinzi wa kutosha.
Hali inakuja baada ya Chirwa kukosa penalti ya mwisho ya Yanga baada ya wenzake wote wanne kupata ambao ni Mkongo Papy Kabamba Tshishimbi, na wazalendo Hassan Ramadhani Kessy, Raphael Daudi Lothi pamoja na Gardiel Michael Mbaga katika mchezo wa nusu fainali uliopigwa jana.
Mshambuliaji wa Kimataifa wa Yanga Mzambia, Obrey Chirwa akiwa amezungukwa na mashabiki wa soka jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo huo Chirwa aliingia kipindi cha pili kwenda kuchukua nafasi ya Pius Buswita ili kuongeza nguvu safu ya ushambuliaji ya Yanga, lakini Mzambia huyo alishindwa kucheza vizuri kutokana na kile kilichoonekana wazi hakuwa fiti.
Chirwa alikuwa kwao Zambia kufuatia mgomo wake wa kushinikiza alipwe fedha za usajili na amerejea juzi Dar es Salaam na moja kwa moja kusafirishwa kuletwa Zanzibar kabla ya kuingizwa uwanjani kipindi cha pili.
Hata hivyo penalti aliyokwenda kupiga ilikuwa ya ovyo kabisa na kipa wa URA hakuhitaji kujisumbua kuiokoa, kwani mpira ulimkuta mikononi tena pale pale aliposimama.
Kocha Msaidizi wa Yanga Shadrack Nsajigwa akizungumza na waandishi wa habari.
Baadhi ya Mashabiki wa soka.
Akizungumza na waandishi wa habari baada kuwasili jijini Dar es Salaam, Kocha msaidizi wa Yanga Shadrack Nsajigwa amesema kuwa kikosi chake kimepambana na kuweza kuishia katika hatua ya nusu fainali.
Amesema kuwa lengo lao lilikuwa ni kuchukua kombe lakini katika mpira lolote linaweza kutokea.
Akizungmuzia mcheza wao wa kimataifa Mzambia Chiwra ambaye alikosa penati ya mwisho na kusababisha kutolewa nje katika mashindano hayo na URA ya Uganda, amesema hakuwa fiti katika mchezo huo.
Amesema kuwa kuna uwezekano siku hiyo hakuwa vizuri kwani katika mchezo lolote linaweza kutokea.
Yanga SC imepanda boti na kurejea mjini Dar es Salaam baada ya kutolewa kwenye michuano ya Kombe la Mapunduzi kwa penalti 5-4 na URA ya Uganda kufuatia sare ya 0-0 ndani ya dakika 90 katika Uwanja wa Amaan, Zanzibar hapa januari 10 mwaka huu.
Hatua hiyo imebainisha kuwa Yanga SC imeendeleza utamaduni wake wa kufanya vibaya kwenye hatua ya matuta baada ya mshambuliaji wake Mzambia, Obrey Chirwa kumdakisha mpira kipa wa URA, Alionzi Nafian.
Chirwa alikosa penalti ya mwisho ya Yanga baada ya wenzake wote wanne, Mkongo Papy Kabamba Tshishimbi na wazalendo Hassan Ramadhani Kessy, Raphael Daudi Lothi na Gardiel Michael Mbaga kufunga.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Issa Hajji, aliyesaidiwa na Shehe Suleiman na Mwanahija Makame, penalti za URA zilifungwa na Patrick Mbowa, Enock Kigumba, Shafiq Kagimu, Jimmy Kulaba na Brian Majwega.
Katika dakika 90 za mchezo timu zote zilishambuliana kwa zamu, ingawa URA ndiyo walioonekana kulitia misukosuko zaidi lango la Yanga.
Kufatia matokea Matajili Azam Fc wataminjana na URA katika mchezo wa fainali utakaopigwa huku visiwani Zanzibar.
No comments:
Post a Comment