WINGU LA HABARI
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Mkurugenzi wa IBRA
Contractors na Rais wa Sauti ya Wanawake
Wajasiriamali Tanzania (VOWET), Maida Waziri akipokelewa katika uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake la Uwezeshaji Kata ya Keko uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wakinamama wa Kata ya Keko wakiwa katika Maandamano uzinduzi
wa Jukwaa la Wanawake la Uwezeshaji katika Kata hiyo.
Mkurugenzi wa IBRA Contractors na Rais wa Sauti ya Wanawake Wajasiriamali Tanzania (VOWET), Maida Waziri akiangalia bidhaa za Wakinamama Wajasiriamali katika Kata ya Keko.
Mkurugenzi wa IBRA Contractors na Rais wa Sauti ya Wanawake Wajasiriamali Tanzania (VOWET), Maida Waziri akiangalia batiki iliyotengenezwa na wakinamama katika Kata ya Keko.
Mtumishi wa benki ya NMB akiwa upande wa kushoto akitoa maelezo kwa Mkurugenzi wa IBRA Contractors na Rais wa Sauti ya Wanawake Wajasiriamali Tanzania (VOWET), Maida Waziri jinsi benki hiyo inavyotoa huduma zake
Mjumbe
Mwamasishaji Jukwaa la Wanawake la Uwezeshaji katika kata Keko na Wilaya ya
Temeke Caroline Sabu akiongea na waandishi wa habari leo jinini Dar es Salaam.
.........
Wanawake
wa Kata ya Keko Wilaya ya Temeke wametakiwa kuwa na umoja wa kufanya kazi za ujasiriamali
jambo ambalo linaweza kuwasaidia kuinua uchumi wa familia zao pamoja na kufanikisha
Tanzania ya Viwanda.
Akizungumza
katika uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake la Uwezeshaji Kata ya Keko Wilaya ya
Temeke, Mkurugenzi wa IBRA
Contractors na Rais wa Sauti ya Wanawake
Wajasiriamali Tanzania (VOWET), Maida Waziri amesema kuwa wakinamama wanapaswa
kuendelea kuwa na mwamko wa kupiga hatua katika safari ya kuelekea Tanzania ya
viwanda.
Waziri
ambaye ni mgeni rasmi katika uzinduzi huo, amesema kuwa kwa jitihada
zinazofanya na wakinamama kata ya keko inanyesha moja kwa moja zinaunga mkono juhudi
za serikali katika kufanikisha tanzania ya viwanda.
“Nimepitia
bidhaa walizotengeneza wakinamama wa kaka ya kek…kiukweli wanapambana sana kwenda
katika tanzania ya viwanda” amesema Waziri.
Hata
hivyo Waziri amefafanua kuwa ataendelea kuwapa ushirikiano wakinamama hao
katika nyanja mbalimbali ikiwemo kuwapa
elimu ya ujasiriamali pamoja na kuwaunganisha na taasisi za fedha kwa ajili ya
kupata mikopo kwa gharama nafuu.
Naye Mjumbe
Mwamasishaji Jukwaa la Wanawake la Uwezeshaji katika kata Keko na Wilaya ya
Temeke Caroline Sabu, amesema kuwa wanawake wanapaswa kuendelea kufanya
biashara mbalimbali ili kupiga hatua katika uchumi.
Amesema
kuwa kwa sasa katika kata ya keko mwitikio ni mzuri kutokana wakinamama kuwa na
mwamko na kufanikiwa kujiunga katika vikindi mbalimbali vya ujasiriamali
Sabu
ameeleza kuwa katika kata ya keko kuna jumla ya vikundi 54 vya wanawake ambavyo
vinajishughulisha na masula ya ujasiriamali kwa kutengezena bidhaa mbalimbali, huku
kila kikundi kikiwa na jumla ya wanawake 30 wenye umri kuanzia 18 na kuendelea.
“Vikundi
hivi vinaunda Jukwaa la Wanawake la Uwezeshaji Kata ya Keko ambapo leo
tumefanya uzinduzi rasmi, lakini idadi ya vikundi inaweza kuongezeka kutokana
wanaweke bado wanaendelea kujiunda katika vikundi” amesema Sabu.
No comments:
Post a Comment